tangazo

Aibu ya hedhi yawalazimisha wasichana kuchukua mbinu mbadala


Wanawake wengi huugua kimya kimyaHaki miliki ya pichaSCIENCE PHOTO LIBRARY
Image captionWanawake wengi huugua kimya kimya

Hedhi ni jambo la kimaumbile na ni sehemu ya maisha ya kila msichana. Lakini umaskini na unyanyapaa wa wa hedhi vimekuwa na athari kubwa kwa maisha ya wasichana na wakati mwingine huathiri elimu yao.
Inakadiriwa kuwa msichana mmoja kati ya wasichana 10 barani Afrika hukosa masomo shuleni wakati wanapokuwa katika kipindi cha hedhi. Ukosefu wa taulo za hedhi na aibu ya hedhi unawalazimisha kutumia dawa za kuzuwia mimba ambazo husitisha hedhi.
Moja ya nchi ambako wasichana hukabiliwa na hali hii ni nchi ya Namibia.
Alipotembelea mji mkuu wa Namibia Windhoek hivi karibuni mwandishi wa BBC Rhoda Odhiambo alibaini kuwa, licha ya kwamba namibia ni moja ya maeno bora zaidi ya kuishi kusini mwa Afrika kulinga na ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu furaha, wanawake na wasichana si watu wenye furaha.

Unaweza pia kutazama:
Haba na Haba: Wajibu wa jamii Tanzania katika kuhakikisha hedhi salama kwa wasichana

Hii ni kwasababu mzunguko wa kila mwezi wa hedhi ambao ni wa kimaumbile unawaathiri zaidi ya wasichana 100, 000 ambao wanaouna kama aibu na kwa hiyo jambo hilo linabaikia kuwa ni la siri.
Nchini Namibia, si kwamba hedhi ni jambo la aibu tu kuwa na hedhi kila mwezi, bali, bali hata wengi miongoni mwa wasichana ni maskini sana wasiokuwa na uwezo wa kununua taulo za hedhi. Mmoja wao ni msichana Namasiku mwenye umri wa miaka 12.
''Nilipopata hedhi kwa mara ya kwanza nilikuwa na uvimbe kooni, nikafikiria labdanimejeruhiwa …mama yangu aliniambia kuwa nimekuwa sasa na kwamba ninapaswa kujijali mwenyewe'', alisema Namasiku.
Na kila mwezi kati ya tarehe 8 na 12 kuficha damu yake ya hedhi.

Dawa za kuzuwia ujauzito hutolewa bure katika hospitali zote za serikali kwa wasichana wanaoshiriki ngono, na walio chini ya umri wa miaka 16 lazima wasindikizwe na wazazi
Image captionDawa za kuzuwia ujauzito hutolewa bure katika hospitali zote za serikali kwa wasichana wanaoshiriki ngono, na walio chini ya umri wa miaka 16 lazima wasindikizwe na wazazi

Alipoulizwa ikiwa mama yake aliweza kumnunulia taulo za hedhi alisema:
''Hapana, hakuweza kuninunulia taulo za hedhi. Aliniambia kuwa ni lazima nikate kipande cha godoro na nikitumie hadi nitakapopata taulo za hedhi. Kama nisipopata magodoro , nitumie karatasi za usafi za msalani au magazeti na wakati mwingine nitumie nguo kuu kuu''.
Kwasababu mama yake Namasiku hana uwezo wa kumnunulia binti yake taulo za hedhi bwakati mmoja alimpeleka katika kliniki ili apewe tembe za kuzuwia ujauzito ili kudhibiti hedhi yake ya kil mwezi.
Ninamshauri binti yangu atumie njia ya mpango wa uzazi. Nilikuwa nikimsindikiza , lakini kwa sasa anasaidiwa. Anapata taulo za hedhi kutoka shuleni na kwa sasa hatumii tembe za kuzuwia uzazi. Anasema Anita mama yake Namasiku.

Wanawake na wasichana hutumia karatasi za chooni wakati wa hedhi
Image captionWanawake na wasichana hutumia karatasi za chooni, magazeti, matawi ya miti na baadhi hulazimika kutumia dawa za kuzuwia ujauzito zinazozuwia hedhi ili kuepuka aibu

Bei ya pakiti moja ya taulo za hedhi ni kati ya dola 1 na dola 3 za Kimatekani . Kwa mnamibia pesa hizo zinatosha kununua mikate miwili na chupa ya mililita 700 ya mafuta ya kupikia. Inakadiriwa kuwa zaidi ya wasichana 150,000 nchini Namibia hawana pesa za kununua taulo za hedhi . Wengi miongoni mwao hutumia vitambaa, vipande vya godoro, matawi ya miti, na baadhi hulazimika kutumia tembe za kuzuwia ujauzito kudhibiti.
Dawa za kuzuwia ujauzito hutolewa bure katika hospitali zote za serikali kwa wasichana wanaoshiriki ngono. Na wale walio chini ya umri wa miaka 16 lazima wasindikizwe na walezi wao au wazazi . Ndapewa mwenye umri wa miaka 17-amekuwa akizitumia kwa muda wa mwaka mmoja sasa kwasababu taulo za hedhi ni ghali mno.
''Kwangu, ninapata hedhi mara tatu kwa mwaka .Tu. Nadhani nimeharibika kwasababu hakuna jinsi mtu anaweza kupata hedhi mara tatu kwa miezi mitatu tu kila mwaka. Si salama kabisa.
Sindano ina homoni aina ya progesterone. Inapoingizwa mwilini , huzuwia kutiungwa kwa mayai ya uzazi kutoka kwenye mfuko wa mayai ya uzazi(ovari), hivyo huingilia mfumo mzima wa hedhi ya mwezi ya mwanamke. Daktari bingwa wa uzazi John Keeisab anasema dawa za kuzuwia ujauzito zilitengenezwa kwa ajili ya kupanga uzazi na sio kudhibiti hedhi.

An Indian man looks on as he walks along a wall painting about menstruation in Guwahati on May 28, 2019Haki miliki ya pichaAFP
Image captionKuna unyanyapaa mkubwa kuhusu hedhi pia India

John Keeisab anasema : Wakati mtu fulani anapokuja kumuona mhudumu wa kliniki, iwe ni katika kliniki au kwa daktari na kusema ninaweza kupata tembe za kuzuwia ujauzito ili nisipate hedhi. Ninafikiri tunahitaji kuwaelimishakwamba dawa hizi hazikuwa na madumuni hayo. Nyingi kati ya dawa hizi zina madharahasa zile anazochomwa mtu , inamaanisha kuwa hatimae hedhi zinaweza kutoweka na mtu akakauka.
Huku kukiwa na kiwango cha juu cha gharama ya taulo za hedhi, wasichana wengi wa Namibia hasa wale wanaoishi katika hali ya umaskini wa kupindukia hawawezi kumudu kununua taulo za hedhi . Waziri wa afya Julieta Kavetuna amekanusha kuwa kuna tatizo la ukosefu wa taulo za hedhi alipoulizwa serikali inafanya nini kuwasaidia wasichana kupata taulo hizo.

Unaweza pia kutazama:
Wasichana wanatumia vikopo vya hedhi kujisitiri

''Ninadhani dhana hiyo imepitwa na wakati kwamba wasichana wanakosa shule kwasababu hawawezi kununua taulo za hedhi , kwasababu labda ni ukosefu wa taarifa au hazitolewi . Sidhani unahitaji hili '', alisema Bi Julieta Kavetuna.
Hata kama jamii inaweza kusema kuwa hili ni tatizo la mwanamke, wasichana wengi wa Namibiakama Ndapewa and Namasiku wataendelea kupata athari za umaskini. lakini kama tatizo hili halitashughulikiwa na serikali wasichana wataendelea kutumia vitu mbadala vya kuzuwia hedhi,na kuipa majina kama roboti nyekundu au mgeni hatari kuelezea hedhi zao, na hivyo kufanya umaskini wa hedhi kuwa mgumu kuukabili.

Post a Comment

0 Comments