Al Ahly waivunjia mbali rekodi ya Yanga


Michezo ya awali ya kuwania kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2019/20 inaendelea na Al Ahly ya Misri wao walicheza mchezo wao wa marudiano Ijumaa hii dhidi ya Atlabara ya Sudan Kusini.

Al Ahly ambao walipata bahati ya michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini kuchezwa kwenye taifa lake kutokana na Uwanja wa Sudan Kusini kuwa katika ukarabati, wamefanikiwa kuifunga Atlabara jumla ya goli 13-0 katika hatua hiyo, mechi ya kwanza wakishinda 4-0 na ya pili ya marudiano iliyochezwa juzi ijumaa wakishinda 9-0.

Ushindi huo unaifanya Al Ahly kufikia rekodi ya Yanga SC ya Tanzania ambayo iliweka rekodi hiyo miaka 10 iliyopita kwa kuifunga klabu ya Etoile d'Or Mirontsy FC ya nchini Comorro kwa tofauti ya goli 13.

Katika raundi hiyo ya awali mwaka 2009 Yanga iliibuka na ushindi wa Jumla ya goli 14-1 dhidi ya Etoile d’or Mironsty kutoka Comorro.

Mchezo wa kwanza walishinda 8-1 akiwa nyumbani na mchezo wa marudiano uliochezwa Moron Comorro wakishinda 6-0 na kufanya idadi ya magoli kuwa 14-1 sawa na utofauti wa mabao 13-0 rekodi ambayo ilidumu kwa miaka 10 na Al Ahly ndio wameifikia Ijumaa hii ya kuwa timu ya pili kuwahi kupita kwa idadi ya 13-0 katika historia ya mashindano hayo.

Post a Comment

0 Comments