tangazo

Bingwa wa mita 800 duniani David Rudisha ahusika katika ajali mbaya ya barabarani Kenya


David Rudisha ahusika katika ajali mbaya ya barabarani

Bingwa wa mbio za mita 800 anayeshikilia rekodi ya dunia David Rudisha anaendelea kupata matibabu kufuatia ajali mbaya ya barabarani ilimuacha akiuguza majeraha .
Bwana Rudisha alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota V8 siku ya Jumapili alfajiri ambapo tairi lake lilipasuka karibu na mji wa Keroke na hivyobasi kugongana ana kwa ana na basi moja lililokuwa likitokea upande wa pili.
Ajali hiyo ya mwendo wa saa nne na nusu ilitokea katika eneo hatari katika barabara kuu ya Kisii Keroka kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya.
Bwana Stephen Ole Marai ambaye ni rafiki a Rudisha na jirani alisema kwamba hali ya mwanariadha huyo haipo hataraini na alitibiwa katika hospitali moja iliopo Keroka kabla ya kuhamishwa katika hospitali ya Kilgoris.
Katika mitandao ya kijamii Wakenya walimwambia pole Rudisha huku wakiweka picha za gari lake lililoharibika vibaya
Bwana Rudisha anatoka eneo la Kilgoris kaunti ya naroko.
Rudisha yuko salama , lakini anauguza majeraha. Tunaondoka Kilgoris kueleka kituo cha polisi cha Keroka ambapo atakutana na maafisa wa polisi, alisema bwana Ole Marai akinukuliwa na gazeti la Daily Nation nchini Kenya.
Gari la Rudisha lililoharibiwa vibaya pamoja na basi hilo yalipelekwa katika kituo cha polisi cha Keroka.
Bingwa huyo mara mbili wa Olimpiki ametoweka katika riadhaa kwa muda mrefu sasa.

Je kwa nini hashiriki riadha?

Alitoweka katika riadha huku akikosa misimu miwili mfululizo kutokana na jeraha ambalo alikua akiuguza, lakini hilo halikuwanyamazisha mashabiki wake duniani ambao wametaka kujua hali yake.
Mwezi uliopita mkewe alichapisha ujumbe katika mtandao wa facebook uliosema: David Rudisha wacha kunisumbua na watoto wangu. Kwa familia yangu moyo wangu una uchungu siwezi kuvumilia tena.
Nawapenda nyote. Ujumbe huo ulionekana kuzua maswali mengi kuhusu familia yake na kutokuwepo kwake katika riadha.
Ajenti wa Rudisha Mitchel Boeting alikataa kutoa tamko lolote kuhusu maswala ya kifamilia ya mwanariadha huyo.
Aliambia gazeti la The Standard nchini Kenya kutoka Amstaerdam : Siwezi kuzungumzia kuhusu maswala yao ya kifamilia Sijui hata kuhusu chapisho hilo.
David huenda asishiriki katika riadha msimu huu. Jeraha lake lilipona na likarudi. Atachalewa kurudi msimu huu na nadhani atarudi msimu ujao. Tunatumaini kwamba kila kitu kitakuwa sawa alinukuliwa na The Standard akisema.
Rudisha ambaye michezo ya Olimpiki ya 2016 katika mita 800 hajashiriki katika riadha michezo ya almasi ya 2017 iliofanyika mjini Shangahi China.

Post a Comment

0 Comments