Ligi ya mabingwa Caf: Yanga yafuzu Simba yaondolewa na UD Songo ya Msumbiji


Je mabingwa hao watafanikiwa kupeperusha bendera ya TanzaniaHaki miliki ya pichaMAHMOUD BIN ZUBEIRY

Timu ya Tanzania yanga SC wamefuzu katika raundi ya pili baada ya kupata ushindi muhimu ugenini siku ya Jumamosi.
Yanga SC wametinga raundi ya pili ya ligi ya mabingwa ya Caf baada ya kuilaza Township Rollers ya Botwana 1-0.
Goli la dakika ya 42 lililofungwa na Juma Balinya ndio lililohitajika na mabingwa hao wa Afrika mashariki kuwalaza wenyeji wao na kusonga mbele katika raundi ya pili kwa jumla ya magoli 2-1.
Kufuatia sare ya 1-1 katika mechi ya awamu ya kwanza iliochezwa nchini Tanzania klabu hiyo ya Botswana ilikuwa na fursa nzuri ya kusonga mbele kwani walihitaji sare tasa kufuzu.

Klabu za Simba na Yanga ndio tegemeo Tanzania

Kwa upande wa Yanga walilazimika kufunga goli ili kuimarisha matumaini yoyote ya kufuzu katika raundi ya pili.
Licha ya kipindi cha kwanza kilichosisimua , hakuna timu ilioona lango la mwengine , lakini walikuwa wenyeji waliokuwa na presha ya kupata ushindi.
Yanga sasa itakabiliana na mshindi kati ya Zesco United ya Zambia, ambao walisonga mbele kwa kuilaza Green Mamba 3-0 kwa jumla ya magoli.

John Bocco ni miongoni ma wachezaji wanaotegemewa kuisaidi SimbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Wakati huohuo mabingwa wa ligi ya Tanzania Simba SC wamejiandaa vilivyo kukabiliana na klabu ya UD Songo ya msumbiji katika mechi nyengine ya ligi ya mabingwa Afrika.
Wachezaji wa Simba Gadile Michael na Francis Kahata wana matumaini makubwa kufuzu katika raundi ya pili katika uwanja wa kitaifa wa Da es salaam siku ya jumapili.
Michael ambaye ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na klabu hiyo msimu huu anaamini maandalizi ya klabu hiyo yatasaidia pakubwa kuwalaza wageni hao.
Baada ya sare tasa ugenini Simba itahitaji ushindi ili kufuzu katika raundi ya pili.

Mechi nyengine za kombe hilo ni

  • JS Kabylie vs Horoya AC
  • Génération Foot vs Zamalek
  • Cõte d'Or 🇸🇨 vs Mamelodi Sundowns
  • Young Africans vs ZESCO United
  • Green Eagles vs 1° de Agost

Post a Comment

0 Comments