London: Maalfu kuandamana kupinga kusimamishwa bunge

Maalfu ya watu nchini Uingereza kote watarajiwa kushiriki kwenye maandamano ya kupinga kusimamishwa kwa shughuli za Bunge.

    
London Anti-Brexit-Plakat (picture-alliance/NurPhoto/D. Cliff)
Maandamano hayo yameitishwa na wapinzani wa Brexit wa kundi linaloitwa "Another Europe is Possible" yaani Ulaya nyingine yawezekana. Malkia Elizabeth wa pili ameridhia hatua ya Waziri Mkuu Boris Johnson ya kulisimamisha bunge hadi katikati ya mwezi Oktoba ambapo zitabakia takriban wiki mbili ambapo Uingereza itapaswa kujiondoa umoja wa Ulaya.
Wachambuzi wanasema ni hila ya serikali kuwanyima wabunge uwezekano wa kuzuia Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya bila ya mkataba.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anakabiliwa na changamoto za kisheria kutokana na hatua yake ya kusimamisha bunge mnamo siku ya Ijumaa. Johnson ametahadharisha juu ya hatua za kuuvuruga mpango wa Uingereza wa kutafuta makubaliano sahihi na Umoja wa Ulaya. Amesema kadiri washirika na marafiki wa Uingereza wanavyozidi kufikiria kwamba mpango wa Brexit unaweza kusimamishwa na nchi hiyo inaweza kuendelea kuwamo kwenye Umoja huo ndivyo matatizo yanavyozidim kujitokeza na kusababisha uwezekano mdogo wa kufikiwa makubaliano yanayohitajiwa na Uingereza
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson (Reuters/D. Martinez)
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Waziri Mkuu wa Uingereza amsema nchi yake kushindwa kuondoka kutoka kwenye Jumuiya ya Ulaya kama walivyochagua wapiga kura kwenye kura ya maoni kutasababisha athari kubwa kwa vyama vikubwa vya kisiasa nchini Uingereza. 
Mapema Ijumaa, mahakama ya Scottland ilikataa ombi la kuzuia maamuzi ya bwana Johnson ya kusimamisha bunge, lakini imeamuru usikilizwaji kamili juu ya suala hilo ufanyike katika siku tatu zijazo.
Wabunge wapatao 75 wa Uingereza walifungua kesi hiyo mjini Edinburgh kupinga hatua ya kusimamishwa bunge. Waziri Mkuu Boris Johnson amesema mapumziko hayo ni muhimu kwa serikali yake ili kuweza kuzindua rasmi ajenda yake kwa mwaka ujao.
Kesi zingine za kisheria zimefikishwa katika mahakama za juu katika miji ya Belfast na London. Waziri mkuu wa zamani wa chama cha kihafidhina John Major amesema Ijumaa anaunga mkono juhudi zilizoanzishwa na mwanaharakati anayepinga Brexit Gina Miller.
Kulingana na serikali, wahusika katika mazungumzo ya Brexit wataanza kukutana  na wenzao wa Umoja wa Ulaya mara mbili kwa wiki mnamo Septemba kama sehemu ya juhudi za kujadili mpango mpya wa Brexit.
Vyanzo:/DPA/AP

Post a Comment

0 Comments