tangazo

Lugha ya Kiswahili inavyokuza sanaa katika mipaka ya Kimataifa


Corona Cermek,na familia yake nchini Jamhuri ya CzechHaki miliki ya pichaCORONA CERMEK

Kiswahili kinazidi kukua na kushamiri kila uchao na kama zilivyoenea lugha za Kiingereza,Kifaransa na Kichina, Kiswahili pia kinandelea kwenda mbali zaidi.
Juma lililopita Lugha hiyo ilitangazwa kuwa lugha ya Nne Rasmi kutumika kwa nchi za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika, SADC
Carona Cermak, ambaye ni mwalimu wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Masaryk nchini Jamhuri ya Czech ameiambia BBC kuwa lugha hiyo imepewa nafasi kama lugha ya kimataifa.
Anasema Kozi ya kiswahili katika chuo hicho hutolewa kwa wanafunzi na watu wote wanaopenda kujifunza kiswahili kwa sababu yoyote.
'Kwa kweli watu wengi wanaopenda kujifunza lugha ya kiswahili ni wanafunzi madaktari na wengine ni wale ambao kutembelea nchi za Kiafrika kama vile Tanzania na wanapenda kujifunza maneno mawili matatu ndio wakifika wawezi kujua ni jinsi gani watazungumza na watuwanaoishi Tanzania,'' anasema Carona Cermak.

Maonyesho mbalimbali ya utamaduni wa mswahili nchini Jamhuri ya CzechHaki miliki ya pichaCORONA CERMEK
Image captionMaonyesho mbalimbali ya utamaduni wa mswahili nchini Jamhuri ya Czech

Kabla ya kozi hiyo kuanza kufundishwa alishirikiana na chuo hicho katika maonyesho mbalimbali ya utamaduni wa mswahili.
Wanafunzi wake wanasomea udaktari, wengine ni watu wanaotembelea sana Zanzibar, pia kuna mwandishi wa vitabu kuhusu Kenya na baadhi ni wafanyabishara katika eneo la Afrika ya mashariki.
''Nafurahi kutangaza kiswahili kwa namna hii, huu ni mwanzo mzuri sana, naamini natengeneza ajira ya kufundisha kiswahili na kutangaza kiswahili,''alisema.
Kando na kufunza kiswahili katika chuo Kikuu nchini Jamhuri ya Cheki, Carona Cermak ni mwalimu wa kingereza wa shule ya chekechea nchini humo.
Anasema kuwa ametumia fursa hiyo kutafsiri kwa kiswahili mambo mengi anayofundisha.
''Naamini tukiweka mkazo kwenye kumwelimisha mtoto kupitia lugha yake mama basi atakuwa mwelewa zaidi, hivyo na mimi nikaona ni vyema mtoto wa Afrika Mashariki afaidike na haya ninayofundisha,''aliongeza Carona.
Kupitia mitandao ya kijamii bi Carona ameweza kuwafikia wazazi, watoto, walimu na wanajamii wengi wa Afrika Mashariki.
''Nimefungua channel ya Youtube, facebook na instagram kushirikisha watu mambo haya mazuri ya mtoto.''

Corona Cermek,Mwalimu wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Masaryk nchini Jamhuri ya CzechHaki miliki ya pichaCORONA CERMEK

Hivi karibuni mwimbaji maarufu nchini Marekani Beyonce aliachia kibao kipya na maneno ya kwanza kabisa ya kibao hicho yalikua kwa lugha ya Kiswahili.
"Uishi kwa muda mrefu mfalme," sauti nyembamba inaimba kisha sauti nzito inaitika "uishi kwa", kionjo hiko kinajirudia mara mbili na kisha wimbo kuendelea kwa Kingereza.
Kibao hicho kiitwacho Spirit ni sehemu ya albamu inayosindikiza filamu mpya ya Lion King inayotengenezwa na kampuni kubwa ya Disney ya nchini Marekani.
Mfalme anayeimbwa kwenye kibao hicho ni Simba dume kijana ambaye anaanza safari ya kupambana ili kuwa mfalme wa nyika.
Filamu ya Lion King, "inajumuisha sauti za kutoka barani Afrika," ilieleza kampuni ya Disney.

BeyonceHaki miliki ya pichaDISNEY

Nchini Tanzania Nash MC ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiswahili na Sanaa mwanaharakati wa kiswahili na msanii wa utamaduni wa Hip hop Tanzania amekuwa akitumia kiswahili kupitisha ujumbe.
Kutokana na juhudi hizo mwaka Uliopita Nash alipata mwaliko kutumbuiza katika Tamasha la African Festival na aliamua kutumia fursa hiyo kuimba wimbo wake wa Kiswahili ambao ulikuwa kivutio kikubwa.
Akizungumza na BBC alisema aliamua kutumia kiswahili kwa sababu ndio lugha ambayo inaongelewa na watu wengi Afrika pamoja na nchi nyingi za Ulaya kiswahili kimeshika sana.
'' Ilikuwa ni lazima nitumia lugha yangu ya nyumbani ili niwafikishie ujumbe watu wa karibu kwa sababu ukiwafikiashia ujumbe watu wa karibu wa mbali watajisogeza wenyewe''
Japo katika muktadha wa lugha msanii yuko huru kuimba lugha ya Kiswahili iliyochanganywa na Kiingereza, Nash MC anawashauri wasani wa kuzingati alugha moja ili wawe tofauti.
''Unapochanganya lugha ni vyema uangalie eneo- ni watu gani wanakuzunguka na wana uelewa kiasi gani kuhusu huo uchanganyaji wa lugha''
Mwanaharakati huyo wa kiswahili anasema wasani wa muziki wana nafasi kubwa sana hatua ya kuikuza kiswahili kimataifa.
Wataalamu wanakadiria kuwa lugha ya Kiswahili kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 100 Duniani.

Post a Comment

0 Comments