MAFURIKO HAYAZUIWI KWA MKONO HAPA KAZI TUU

Air Tanzania: Mjadala waibuka baada ya ndege ya Tanzania kuzuliwa Afrika Kusini


Ndege ya Air TanzaniaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Hatua ya Mahakama kuu ya nchini Afrika Kusini kuzuilia kuruka ndege ya Air Tanzania imeendelea kuzua mjadala kuhusu chanzo chake.
Mpaka sasa Mamlaka nchini Afrika Kusini haijatoa tamko lolote kuhusiana na hatua hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa inatoka Afrika Kusini kwenda jijini Dar es Salaam.
Lakini Kwa mujibu wa balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ndege hiyo imezuiliwa kwa amri ya Mahakama Kuu ya mjini Johannesburg.
Ripoti ya baadhi za vyombo vya habari nchini Tanzania zinaashiria kuwa abiria waliokuwa ndani ya ndege ya Air Tanzania iliyozuiliwa kuondoka katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo mjini Johannesburg wametafutiwa usafiri mbadala katika nmashirika mengine ya ndege.
Gazeti la Mwananchi linaripoti kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Ladislaus Matindi amesema ''Kuna safari nyingi zitakazoathiriwa kutokana na kushikiliwa kwa ndege hiyo aina ya Air Bus A220-300''
Bwa. Matindi ameliambia Mwananchi kuwa abiria waliokata tiketi wataarifiwa iwapo kutakuwa na mabadiliko yoyote ama ipo kama ilivyopangwa.
Tayari Shirika hilo limetoa taarifa rasmi kupitia mtandao wake wa Twitter kuwaomba radhi wateja wake na kuongeza kwamba kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake itafanyia marekebisho safari zake.
Msemaji wa Mkuu wa serikali ya Tanzania ameiambia BBC kuwa wanasheria wa nchi hiyo wamewasili nchini Afrika Kusini kufuatilia suala hilo na kwamba wakikamilisha mchakato huo watatoa taarifa kamili.
Taarifa iliyotolewa Ijumaa usiku na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk Leonard Chamuriho ilieleza kuwa serikali kupitia ofisi ya mwanasheria mkuu inafuatilia suala hilo.

Taarifa ya serikaliHaki miliki ya pichaWIZARA YA UCHUKUZI TANZANIA

Baadhi ya raia nchini Tanzania wamekuwa wakijadili nini huenda imeeifanya mahakama ya Afrika Kusini kuzuia ndege hiyo.
@majanimabichi ameandika katika Twitter yake akiuliza: Kwa nini mahakama ikamate/izuie ndege? Kuna jambo limejificha nyuma ya pazia. Toeni sababu.
@PaternusP aliandika:Tulitazame kwa umakini na kidiplomasia. Kutikiswa lazima watatutikisa kutupima REACTIONS zetu. Hakuna haja ya kupaniki juu ya jambo hili. Adapt, Improvise, Overcome.
@catfish88854732 aliandika South Africa ; mahakama ziko huru .Rais wa Sauzi kamwe hawezi kuingilia mahakama.
Wengine walichukua jukumu la kuwafafanulia wenzao maana ya hatua hiyo
Shirika la ndege la Tanzania linalomilikiwa na serikali lilizindua safari yake ya kwanza kwenda mjini Johannesbur, Afrika Kusini mwezi Juni mwaka huu katika hatua ambayo lengo lake lilitajwa kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini ulifikiwa mwaka 2002 baada ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini kununua hisa za Shirika la Ndege la Tanzania.
Lakini ushirikiano huo ulimalizika baada ya serikali ya Tanzania kununua hisa za Shirika la Ndege la Afrika Kusini ili kumiliki Shirika hilo kwa 100%.

AirTanzaniaHaki miliki ya pichaIKULU

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Global Travel Industry, miaka miwili baadae Shirika la ndege la Afrika Kusini liliwasilisha kesi mahakamani mjini Dar es Salaam katika jaribio la kutaka kulipwa deni lake la dola milioni 4.1 lililokuwa likiidai ATCL.
Juhudi za serikali za kuliongezea mtaji Shirika hilo muda mfupi baada ya kuajitennga na SAA bado hazijaleta tija baada ya ATCL kushindwa kupata faida kama ilivyo ahidi.
Kutokana na matukio ya kibiashara yaliopia Mamlaka ya Air Tanzania ilionywa na Bunge kuwa makini zaidi katika ushirikiano wake wa kibiashara na Shirika la Ndege la China , likisema mpago huo unastahili kuwafaidi wafanyikazi wake na Watanzania wote kwa jumla.

Post a Comment

0 Comments