tangazo

Majimbo mawili ya mashariki mwa Ujerumani yapiga kura

Uchaguzi katika majimbo mawili ya Brandenburg na Saxony mashariki mwa Ujerumani ni mtihani mkubwa wa kisiasa kwa serikali ya mseto inayoongozwa na Kansela Angela Merkel.

Wahlplakate zur Landtagswahl in Brandenburg (picture-alliance/dpa/C. Soeder)
Uchaguzi katika majimbo mawili ya mashariki mwa Ujerumani, Saxony na Brandenburg, unafanyika leo Jumapili. Matokeo ya chaguzi katika majimbo hayo ya iliyokuwa zamani Ujerumani Mashariki, yanasubiriwa kwa hamu na nchi nzima. Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia AfD  maarufu kama "Chaguo mbadala kwa Ujerumani” kinatarajiwa kupata ushindi na matokeo ya uchaguzi huo yanaweza kuwa ya kihistoria.
Wapiga kura katika majimbo hayo mawili ya mashariki mwa Ujerumani, wanapiga kura leo Jumapili kuwachagua wabunge wao.
Matokeo ya uchaguzi huo wa bunge hayataamua tu serikali zao za majimbo zitakazokuwa madarakani kwa muda miaka mitano ijayo lakini yanaweza pia kuwa na athari katika kiwango cha kitaifa, na kuleta mabadiliko katika historia ya kisiasa kwenye majimbom haya mawili ya zamani iliyokuwa Ujerumani Mashariki.
Je! Kura hii inamaanisha nini kwa serikali ya mseto inayoongozwa na Kansela Angela Merkel?
Uchaguzi wa serikali za majimbo utakuwa ni mtihani wa kupimana nguvu kwa jumla. Jimbo la Brandenburg ni ngome ya chama cha SPD na Saxony ni ngome ya chama cha Kihafidhina, CDU.
Vyama hiyi vya CDU na SPD vinatarajiwa kushindwa vibaya katika uchaguzi huu wa Jumapili hali ambayo inaweza kuleta athari  na hata kusababisha kuanguka kwa serikali ya mseto iliyopo madarakani. Hii haimaanishikwamba utafanyika uchaguzi mpya, hata hivyo chama cha CDU cha Kansela Angela Merkel kitajikuta kina unda serikali yenye wingi mdogo wa viti.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (Reuters/W. Rattay)
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Viongozi wa vyama vya CDU na SPD katika ngazi ya shirikisho wamependekeza kufanyike tathmini ya kipindi cha kati kuangalia hali tete iliyopo katika serikali ya mseto kufikia katikati ya mwezi Oktoba.
Matokeo mabaya katika uchaguzi unaofanyika Jumapili yanaweza kuwa kishawishi cha mseto huo kuvunjika.
Kura ya maoni yaonyesha chama cha Kijani kitapata zaidi ya asilimia 10
Chama cha watetea mazingira cha Kijani kinatarajiwa kupata matokeo mazuri katika uchaguzi wa leo Jumapili kwenye majimbo yote mawili ya Brandenburg na Saxony. Lakini inapasa kutiliwa maanani kwamba kinakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia AfD.
Mafanikio mapya ya chama cha Kijani katika eneo la mashariki mwa Ujerumani, katika majimbo ya Brandenburg na Saxony pia yanaweza kuongeza chachu katika uchaguzi ujao wa shirikisho, na nafasi pia kutoa nafasi kwa chama cha Kijani ya kuongoza serikali ya shirikisho.
Katika jimbo la tatu la eneo hilo la mashariki, Thüringen, ambalo litapiga kura mwishoni mwa mwezi wa Oktoba chama cha Kijani kimekuwa kwenye serikali ya mseto inayongozwa na Chama cha SPD tangu mwaka 2014. Katika eneo la Saxony-Anhalt, hivi sasa chama cha Kijani kimo kwenye serikali ya mseto na vyama vya CDU na SPD.
Vyanzo:/DPAE/ Permalink https://p.dw.com/p/3OoT5

Post a Comment

0 Comments