tangazo

Nyimbo maarufu ''Tetema'' na ''Wamlambezi'' zapigwa marufuku nje ya vilabu

Mkurugenzi wa Bodi ya udhibiti wa viwango vya filamu nchini Ezekiel Mutua
Image captionEzekiel Mutua ( kulia) amesema ''Wamlambez'' na ''Tetema'' ni nyimbo za ponografia
Mkuu wa bodi ya udhibiti wa maudhui ya filamu nchini Kenya (KFCB) Dkt Ezekiel Mutua amezuwia kuchezwa kwa nyimbo za Rayvanny 'Tetema' na ' 'Wamlambez' kwenye mikusanyiko ya burudani.
Kupitia taarifa yake aliyoitoa kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mutua amezitaja nyimbo hizo kama ' ponografia halisi,' akisema kuwa zitaruhusiwa kuchezwa tu kwenye baa na vilabu.
Mutua amezitaja kamakitendo cha 'aibu ' kwa viongozi wa kitaifa wanaodaiwa kudensi nyimbo hizo hadharani.
"Nyimbo za Tetema na Wamlambez zinazuiwa kuchezwa nje ya vilabu na baa. Inatia aibu kuwaona hata viongozi wa kitaifa wakidensi na kuimba nyimbo za aibu mbele ya hadharani.
Dr mutuaHaki miliki ya pichaDR ALFRED MUTUA/ FACEBOOK
"Maneno katika nyimbo hizo ni uchafu na hayafai kusikilizwa hadharani hususan mahali ambapo kuna watoto wanaoweza kuwa wanasikiliza maneno au kuona mtu akicheza. Nyimbo zote mbili ni ponografia halisi ," ameandika bwana Mutua.
"Japo hatuzipigi marufuku kwasababu zinaimbwa kwa mtindo wa mafumbo , ni muhimu kwa umma kufahamu kuwa nyimbo hizi ni chafu, na hazifai kuchezwa mahala penye mchanganyiko wa watu wa rika tofauti. Acha zipigwe kwenye vilabu , kwa ajioli ya watu wazima pekee !" aliandika.
Hata hivyo haijafahamika ni vipi agizo la Bwana Mutua litatekelezwa na bodi ya udhibiti wa maudhui ya kiusanii. Baadhi ya Wakenya wamepeleka hisia zao kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na kupigwa marufuku nyimbo hizi katika maeneo mengine nje ya vilabu na baa:
Nae Kelly Simba anasema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa kile zekiel Mutua anachokisahau kila mara ni kwamba huwezi kuzuwia muziki katika karne ya 21 . Akiongeza kuwa ''Wamlambez haiwezi kuzuwiwa kwasababu ni kujieleza kwetu. Eti ni ponografia, ninamaanisha kuwa kati ya wavuti kuu 10 nchini kenya , 3 ni za ponografia'' anasema Kelly Simba kwenye ujumbe wa Twitter
Akizungumza na BBC, Meneja wa Sailors-Mwalimu Racheal amasema uamuzi uliotolewa na Bwana Mutua ni mtazamo wake binafsi na kuongeza kuwa kila wimbo duniani huwa na sehemu ya mafumbo na anasema ''Wamlambezi'' uliimbwa kwa kuzingatia taratibu zote za kimuziki. Sailors Wameahidi kuendelea kutoa nyimbo kwa ajili ya mashabiki wao:
Kikundi cha wanamuziki wa Sailors kilichoimba wimbo Wamlambez, kinasema kitaendelea kutoa nyimbo mpya kwa ajili ya mashabiki wao licha ya Wamlambez kupigw amarufukuHaki miliki ya pichaSAILORS
Image captionKikundi cha wanamuziki wa Sailors kilichoimba wimbo Wamlambez, kinasema kitaendelea kutoa nyimbo mpya kwa ajili ya mashabiki wao licha ya Wamlambez kupigw amarufuku
Hii si mara ya kwanza kwa Bwana Mutua kupiga marufuku nyimbo za wasanii hususana wa muziki wa kizazi kipya kwa madai kwamba maudhui ya nyimbo zao yamejaa matusi, phonografia na yasiyokuwa na maadili.
Mwezi Aprili Bwana Utua alipiga marufuku wimbo Takataka, ambao alisema kuwa unawatusi wanawake.
Bwana Mutua aliuelezea wikmbo huo ulioimbwa na msanii Alvin almaarufu Alvindo uliozalishwa na kampuni ya FastCash Music Group kama wa kishamba na wenye matusi na kuongeza kuwa " kama watu wanaowajibika hatuwezi kuukubali ."
Diamond Platnumz na Rayvanny pia waliwahi kufungiwa kazi yaoHaki miliki ya pichaDIAMONDPLATNUMZ INSTAGRAM
Licha ya kupigwa marufuku nchini Kenya, kwenye ukurasa wake wa Instagram mmiliki wa kampuni ya muziki ya Wasafi- Diamond Platnumz, kwenye ujumbe wake wa Instagram Jumanne amesifia kuendelea kuvuma kwa wimbo ''Tetema'':
Katika miaka ya hivi karibuni wanasanii katika mataifa ya nchi za Afrika mashariki wamekuwa wakikabiliwa na hatua za mamlaka husika na maudhui ya muziki na kuwekewa marufuku ya kazi zao. Nchini Tanzania Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) liliwawafungia kazi zao wanamuziki nyota wa Bongo flava Diamond Platnumz na Rayvany baada ya kutumbuiza kibao kilichofungiwa: Mwezi Disemba wakati Basata ikiwaangushia rungu wasanii hao ilidai kuwa
Uamuzi wa Basata ulifuatia kitendo cha wasanii hao kutumbuiza jukwaani kibao kilichopigwa marufuku na mamlaka cha Mwanza.

Unaweza pia kutazama:

Msafiri Zawose, kijana anayeenzi muziki wa asili Tanzania


Post a Comment

0 Comments