tangazo

Putin, Erdogan wakutana kuzungumzia Syria

Rais wa Urusi Vladimir Putin amekutana na rais wa Uturuki Erdogan wakati mashambulizi Syria yakielekezwa katika  jimbo linaloshikiliwa na waasi la Idlib ambako nchi hizo zimetenga eneo lisilokuwa na shughuli za kijeshi.

    
Russland Zhukovs | MAKS 2019 | Erdogan & Putin (picture-alliance/dpa/Tass/A. Nikolsky)
Mkutano  wa  viongozi  hao  mjini  Moscow unafanyika  siku  moja  baada  ya  Erdogan  kusema  Uturuki  iko tayari  kutuma  majeshi  ya  ardhini  kaskazini  mwa  Syria, haraka iwezekanavyo ili kuuweka  salama mpaka. 
Russland Zhukovs | MAKS 2019 | Erdogan & Putin (picture-alliance/AP/M. Shipenkov)
Rais Recep Erdogan wa Uturuki (kushoto) na rais Vladimir Putin (kulia) katika mazungumzo mjini Moscow
Ghasia  zinazoongezeka  katika  jimbo  la  Idlib  zimevuruga makubaliano  yaliyofikiwa  mwezi  Septemba  kati  ya  Urusi na Uturuki  ya  kutenga  eneo  lialotenganisha  majeshi  ya  nchi  hizo mbili. Msafara wa  magari  ya  jeshi  kutoka  Uturuki  ulishambuliwa katika  eneo  la  kaskazini  magharibi  mwa  Syria  juma  lililopita licha ya  Urusi  kutaarifiwa  kuhusu  msafara  huo, wizara  ya  ulinzi  ya Uturuki  imesema.
Uturuki  wakati  huo  huo  inafanyakazi  pamoja  na  Marekani kutenga  eneo  litakalokuwa  na  usalama , karibu  na  mpaka  na Syria , kuwaondoa  wapiganaji   wa  Kikurdi  nchini  Syria wanaoungwa  mkono  na  Marekani  katika  eneo  hilo  na  kuzuwia mmiminiko  wa  wakimbizi wanaoingia  Uturuki.
Russland Zhukovs | MAKS 2019 | Erdogan & Putin (picture-alliance/AP/Presidential Press Service)
Rais Vladimir Putin pamoja na rais wa Uturuki Erdogan wakikagua mfumo wa kijeshi katika maonesho ya kimataifa ya usafiri wa anga MAKS-2019
Uturuki  inaunga  mkono  waasi  wa  upinzani  wanaopambana kutaka  kumuondoa  madarakani  rais Bashar al-Asad, ambaye  jeshi lake , likiungwa  mkono  na  ndege  za  kivita  za  Urusi  lilianza mashambulizi  dhidi  ya  waasi  jimboni  Idlib mwezi  wa  Aprili.
Majeshi ya  Syria
Majeshi  ya  Syria  hivi  karibuni  kabisa  yalichukua  tena  udhibiti wa  mji  wa  Khan Sheikhoun,  mji  mkubwa  zaidi  kusini  mwa  Idlib, ambao  uko  katika  barabara  kuu  ya  kimataifa  inayounganisha Aleppo  na  Damascus.
Mashambulizi  dhidi  ya  Idlib  ni  kitisho kwa  majeshi  ya  Uturuki yaliyoko  katika  vituo  vya  uangalizi. Uturuki  ina  vituo 12  vya uangalizi  katika  jimbo  hilo, na  licha  ya  kusongambele  kwa majeshi ya  Syria, imesema  vituo hivyo  vyote vitabakia.
Putin  na  Erdogan walikutana  kwanza  leo  katika  ufunguzi wa maonesho  ya  vyombo  vya  anga  yanayojulikana  kama  MAKS katika  eneo  la  Moscow, tukio  la  kila  baada  ya  miaka  miwili la viwanda  vya  kutengeneza  ndege.
Rais Vladimir Putin  alisema.
Russland Zhukovs | MAKS 2019 | Erdogan & Putin (picture-alliance/AP/Presidential Press Service)
Rais wa Uturuki Recep Erdogan akisikiliza maelezo kutoka kwa rais Vladmir Putin wakati wakikagua ndege wakati wa maonesho ya MAKS
"Nafikiri  washirika  wetu wote  wa  nje  na  bila  shaka  marafiki wetu  wa  Uturuki, ujumbe  wa  Uturuki, watahamasika  na  mafanikio ya  viwanda  vya  ndege  vya  Urusi pamoja  na  uwezo wa teknolojia ya  jeshi  la  anga  la  Urusi katika kizazi cha  sasa."
Uturuki  mwezi  uliopita ilinunua  mfumo wa  kisasa  wa  makombora chapa S-400 kutoka  Urusi , na  kuzusha hasira  miongoni  mwa wanachama wenzake  wa  jumuiya  ya kujihami  ya  NATO.


Post a Comment

0 Comments