tangazo

Shule waliofungwa Waliompiga Mwingereza

Kenya: Shule ambayo zamani ilikuwa kambi ya wafungwa wa Uingereza1952: Washukiwa wa Mau Mau katika kambi ya gereza nchini Kenya(1952–1960), pia walifahamika kama Mau Mau Rebellion,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMaelfu ya wapiganiaji uhuru wa Kenya walizuiliwa katika kambi hizi
Presentational white space

Katika shule moja eneo la katikati mwa Kenya kuna majengo madogo ambayo wakati mmoja yalitumiwa na wakoloni kama vyumba vya kuwazuilia na kuwatesa wafungwa.
Japo maneno yalioandikwa ''chumba cha mateso yamechakaa bado ni kumbukumbu ya kile kilichokua kikifanyika.
Wambugu wa Nyingi mwenye umeri wa miaka 91 hahitaji kukumbushwa matukio hayo.
Seli hiyo ndogo ni sehemu ambayo alifungiwa kwa miezi mitatu mwaka 1959.
Hakukuwa na kitanda lakini kulikua na ndoo ambayo ilitumika kama choo katika chumba cha futi nane na hakuruhusiwa kutoka nje ya chumba hicho wala kuwasiliana na mtu yeyote.
Sehemu hiyo kwa sasa ni shule ya upili ya Mweru, miaka 60 iliyopita ilikuwa kambi ya Mweru, moja ya mtandao wa zaidi ya kambi 50 za kuzuilia watu nchini Kenya.
Katika kambi hizo washukiwa wa wapiganaji wa Mau Mau walizuiliwa na kuteswa na serikali ya kikoloni.


Composite of Wambugu wa Nyingi now and as a young manHaki miliki ya pichaWAMBUGU WA NYINGI/BBC
Image captionWambugu wa Nyingi, miaka 60 iliyopita na alivyo leo. Alifungwa kwenye zaidi ya kambi 12.

Wapiganaji wa Mau Mau walizindua vita vya kuvizia mwaka 1952 ili kukomboa ardhi yao iliyonyakuliwa na walowezi wa kizungu baada ya Uingereza kutengeneza himaya ya Afrika Mashariki mwaka 1895.
Serikali ilijibu kwa kutangaza hali ya hatari na kuwakamata na kuwazuilia maelfu ya wanaume katika makambi kadhaa maalum.
Kufikia kilele cha operesheni hiyo watu zaidi ya 70,000 walikuwa wametiwa nguvuni.

Waliokuwa kizuizini

Mau Mau walishindwa kijeshi mwaka 1956, baada ya mmoja wa viongozi wao, Dedan Kimathi, kukamatwa na baadae kunyongwa.
Lakini hali ya hatari iliyodumu kwa miaka mitatu ilikomeshwa Kenya ilipopata uhuru wake mwisho wa mwaka 1963 na baadahi ya wanahistoria wanasema kuwa wapiganaji wa Mau Mau walichangia kukomesha uongozi wa kikoloni.


Chumba cha mateso wakati wa ukoloni bado kipo shuleni
Image captionChumba hiki kidogo ambacho kilikuwa katika kambi ya kuzuilia watu tangu zama hizo bado kiko katika shule hiyo
Presentational white space

Bw. wa Nyingi ni mmoja wa watu walioshukiwa kula kiapo cha Mau Mau. kutoka mwaka 1952 hadi 1959 alihamishwa kutoka kambi moja hadi nyingine na hatimaye akaishia kuzuiliwa Mweru kabla ya kuachiliwa huru.
Kwa sasa ana matatizo ya kutembea kutokana na mateso na kazi ngumu alizofanyishwa wakati alipokua kizuizini.
Pia anakumbuka kunyimwa chakula makusudi na kupigwa hadi kupoteza fahamu katika kile baadae kilijulikana na mauaji ya halaiki ya Hola mwaka 1959.


Presentational white space

Jumla ya wafungwa kumi na mmoja wa kambi ya hola waliuawa na walinzi. Japo wa Nyingi, baadae alipata fahamu tayari alikuwa amepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti kwa kudhaniwa amefariki.
Yote ilikua katika juhudi ya kumfanya akiri kuwa ameachana na imani ya kupigana dhidi ya wakoloni.
Inaaminiwa kuwa zaidi ya wapiganaji 20,000 wa Mau Mau waliuawa vitani huku raia 1,800 wakiafrika na walowezi 32 wa kizungu pia walifariki kwa mujibu wa mwanahistoria David Anderson.
Kulikuwa na vifo vingine vingi vilivyotokana na mateso na magonjwa katika kambi za wakoloni.

Kuhifadhi seli hizo

Mwaka 2013, baada ya malumbano ya muda mrefu ya kisheria yalioongozwa na baadhi ya mashujaa wa Mau Mau, akiwemo Bw. wa Nyingi, serikali ya Uingereza ilikiri kuwa "Wakenya walinyanyaswa na waliteswa" na kusikitika kuwa "mateso hayo yalitekelezwa".
Maelfu ya watu walilipwa fidia.


'Picha ya angani ya kambi ya Hola 'iliofungwa'' ambako wapigananji wa Mau Mau waliokataa kushirikiana na serikali ya kenya walizuiliwaHaki miliki ya pichaNATIONAL ARCHIVES
Image captionJumla ya wafungwa 11 waliuawa katika kambi ya kijijini ya Hola mwaka 1959
Presentational white space

Katika shule ya upili ya Mweru, ambako Bw. wa Nyingi alizuiliwa kuna jengo ambalo lilikuwa seli ya kuzuilia wafungwa.
Kwa sasa seli hiyo ni darasa lakini seng'enge iliyochakaa bado inaonekana juu ya ubao kupitia mwanya uliopo kati ya ukuta na paa la mabati ni ishara ya kazi yake ya awali.
Kuna majengo mingi ya kisasa katika shule hiyo kwa sasa na kama anavyosema naibu mkuu wa shule Patrick Karaya, hawastahili kutumia seli ya zamani kama darasa. Lakini anajitolea kulinda majengo machache iliyojengwa tangu miaka ya 1950.
"Tuliamua kwamba ni lazima zisalie zilivyo," alisema. "Watu wengine huenda wakafikiria ni mwiko [kwamba hii ilikuwa kambi ya wafungwa wa Mau Mau], lakini wakija kuiona tunawashauri waziguse ili wafahamu kuwa ni viti vya kweli.
Kuna mpango wa kudumisha kumbukumbu ya eneo hilo zaidi ya kuzuru shule hiyo.


Barbed wire
Image captionMoja ya darasa ya shule ya upili ya Mweru iliyotumika kama seli ya Mau Mau inaonesha sing'eng'e iliyotumiwa wakati huo

Kundi la watuwaliojitolea kutoka ndani na nje ya nchi wamekuja na wazo la kuvigeuza vyumba hivyo kuwa makavazi ya Ukoloni wa Uingereza (MBC) na tayari wamejenga kambi ya kidijitali ya 3D ya kambi hiyo. Wageni wanaotaka kutembelea kambi hizo mtandaoni wanapata fursa ya kujionea mijengo hiyo mtandaoni.
Makavazi hayo ambayo yanapatikana mtandaoni tu, imepewa jina la "historia ya marejesho". Katika tuvuti yake inajielezea kama sehemu ya kujaza pengo ya sehemu ya kihistoria badala ya "kuharibu, kuficha au kubomoa ".
Historia hutegemea vitu vinavyoonekana, ushahidi ulionakiliwa, na kumbukumbu ya watu kuhusu matukio yaliyopita.
Lakini mara nyingine pia inategemea utashi wa maafisa kutaka historia hiyo kusimuliwa, bila ya kufanya hivyo ushahidi unaweza kupotea kama hautaangaziwa.


Vyomba vya mateso nyakati za ukoloni zilivyojengwa upya kupitia mfumo wa kidijitaliHaki miliki ya pichaMBC
Image captionKatika ujenzi mpya wa kidijitali, watazamaji wanaweza kuona mijengo hiyo kutoka ndani na nje kama walivyojionea walipofika eneo hilo

Serikali ya Uingereza huenda iliharibu au kupotosha nyaraka zilizoangazia mateso yaliotekelezwa katika kambi hizo, Bw. Anderson anasema.
Serikali iliyoingia madarakani baada ya Uhuru kupatikana pia haikutaka kusherhekea vugu vugu hilo hatari kwa kuhofia huenda ikatishia malengo ya taifa, mwanahistoria wa Kenya Vincent Simiyu anasema.
Kenya na Uingereza zilichangia kwa kiwango fulani kufutwa kwa historia ya Mau Mau ni matukio waliokumbana nayo.
Sio kwamba mateso waliopitia haikujulikana suala kuu ni kwamba maafisa hawakuzungumzia kadhia yao hadharani.


Brick with initials MWC on it
Image captionBaadhi ya nyumba za udongo ya kambi ya Mweru ambayo wafungwa walilazimishwa kujenga bado zinaonekana shuleni hapo

Mzozo wa Mau Mau na harakati pana ya kupambana na ukoloni ni sehemu ya mtaala wa shule nchini Kenya, lakini mwanaharakati wa kujitolea wa MBC Chao Tayiana aliye na miaka 26 anasema hakuridhika na kile alichojifunza shuleni
"Licha ya kukulia Kenya na kupitia mfumo wa elimu bado nilikuwa na ufahamu mdogo juu ya mapambano ya uhuru," anasema.
Kinachompatia motisha yeye na wenzake ni kuunda mfumo wa 3D wa kambi hizo ambayo inaweza kupatikana mtandaoni
Tulianzia kambi ya Mweru na Aguthi ambazo ziko karibu, na sasa tunaangazia shule ya upili ya wasichana ya Kanguburi, ambako ushahidi wawa seli hizo ungalipo.
'kusahau yaliopita'
Mwezi Agosti mwaka 1963, aliwahakikishia wazungu aliowahutubia kuwa hana kinyongo na mtu na kwamba"hana nia ya kuangazia yaliopita. Tumesamehe yalioptokea zamani".
Katika tukio lingine aliwataja Mau Mau kama "majambazi", mwanahistoria Anderson alisema. Baada ya miongo kadhaa aliandika kuwa, Kenyatta alielezea Mau Mau kama "kama ugonjwa uliotokomezwa na ambao haufai kutajwa tena".
Kitendo cha kusahaulika kwa mchango wa Mau Mau kilichangiwa na serikali huru ya Kenya baada ya mafisa wake kupiga marufuku kundi la Mau Mau hadi mwaka 2003.
Hii inamaanisha wale waliopigania Mau Mau hawakuweza kusimulia waziwazi na hapakuwa na makumbusha ya umma.


Jomo Kenyatta siku ya UhuruHaki miliki ya pichaAFP
Image captionJomo Kenyatta alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kenya mwezi Disemba mwaka 1963

Hadi mwaka 2003, kukiri kuwa mwanashama au kusikika ukizunguza kuhusu Mau Mau ilimaanisha "ungelifungwa jela", alisema Bw wa Nyingi.
Kutoka wakati huo kumekuwa na na gumzo la kutaka mchango wake utambuliwe japo suala la ni mchango upi hasa limekuwa likijadiliwa na wanahistoria.
Kwa upande wake Bw. wa Nyingi anataka Mau Mau watambuliwe kama watu "waliopigania haki na madaraka bila kutumia silaha za kitaalamu".
Akisimama karibu na moja ya mijengo katika shule ya Mweru, Bw. Maina, kutoka makavazi ya eneo hilo, anataka serikali iwahakikishie ulinzi wa mijengo ya kale katika kambi zote.
"Mijengo hii ni ishara ya jinsi mababu zetu walivyoteseka wakipigania uhuru wa taifa letu huku baaadhi yao wakifariki katika seli hizi," alisema.
"Watu wanastahili kujua kwamba uhuru wa nchi hii ulipiganiw [na] watu walimwaga damu."

Post a Comment

0 Comments