Sudan: Abdalla Hamdok ateuliwa kuwa Waziri Mkuu



Abdalla Hamdok addresses the media following his swearing in at the presidential palace in Khartoum, Sudan, 21 August 2019Haki miliki ya pichaThe world
Image captionAbdalla Hamdok alikuwa anafanya kazi Umoja wa mataifa

Sudan imemteua Waziri Mkuu mpya ikiwa nchi hiyo ikiwa kwenye utawala wa mpito wa miaka mitatu chini ya uongozi wa jeshi .
Waziri Mkuu Abdalla Hamdok anasema kuwa kipaumbele chake ni upatikanaji wa amani na kutatua changamoto ya kiuchumi .
Uteuzi wake umekuja wakati ambapo Luteni Abdel Fattah Abdelrahman Burhan alichaguliwa kuwa kiongozi mpya wa baraza huru.
Serikali mpya itaongoza taifa hilo mpaka kipindi cha uchaguzi.
Kumekuwa na vurugu kwa miezi kadhaa ambayo imesababisha vifo vya waandamani wengi.
Upande wa upinzani una matumaini kuwa uteuzi mpya utaweza kusaidia kumaliza utawala wa kijeshi.
Migogoro nchini Sudan ilianza kwa waandamanaji mwishoni mwa mwaka jana wakati ambapo Omar al- Bashir alipoondolewa madarakani baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 30.
Bwana Hamdok ameapishwa kama waziri mkuu wa mpito alipowasili kutoka Ethiopia, eneo alilokuwa akifanyia kazi kama mtaalamu wa uchumi wa umoja wa mataifa(UN) tangu mwaka 2011 kabla ya kuacha kazi hiyo mwaka jana.
"Vipaumbele vya kwanza vya serikali ni kusitisha vita, kuimarisha usalama, kuuza uchumi na kujenga uhusiano mzuri na sera za mataifa ya kigeni," aliwaambia waandishi wa habari.
Mwaka jana, Hamdok alichaguliwa na Bashir kushika nafasi ya waziri wa fedha lakini alikataa, shirika la habari la AFP.
Kuapishwa kwa Hamdok na uwepo wa baraza huru inaonyesha utofauti kwa mara ya kwanza tangu Sudan ikiwa haipo chini ya utawala wa kijeshi tangu Bashir aingie madarakani mwaka 1989 .
Baraza huru inachukua nafasi ya utawala wa mpito wa majeshi wakati ambapo utawala wa kiislamu ulipoondolewa baada ya maandamano makubwa.
Gen Burhan atawaongoza viongozi sita wa kiraia na wengine wanne wa kijeshi kama mpango wa wa muda mrefu wa miezi 39 kuelekea kwenye demokrasia.

Abdalla Hamdok ni nani?
  • Alizaliwa mwaka 1956 nchini Sudan katika jimbo la Kordofan
  • Ana shahada ya uzamivu ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Manchester
  • Mwaka 1990 alifanya kazi kama mshauri mkuu katika shirika la kazi la kimataifa nchini (ILO)Zimbabwe na baadaeakawa mkuu wa sera za uchumi katika benki ya maendeleo ya Afrika(African Development Bank) nchini Ivory Coast
  • Hamdok alifanya pia kama katibu mkuu msaidizi wa tume ya uchumi ya Umoja wa mataifa toka Novemba 2011.

Wamefikaje hapo?
Tarehe 4 mwezi agosti, jeshi na waandamanaji walisaini mkataba wa azimio la kuipa mwanya kuundwa kwa serikali ya mpito. Makubaliano hayo yalisainiwa Agosti 17.


Women celebratingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Walikubaliana na mambo yafuatayo:
  • Watashirikiana katika madaraka kwa miezi 39
  • Uchaguzi utafanyika baada ya kipindi hicho
  • Kuanzishwa kwa baraza huru,baraza la mawaziri na kamati na bodi ya watunga sheria
  • Mkuu wa jeshi ataongoza baraza hilo kwa miezi 21 ya mwanzo, na miezi mingine 18 itaenda kwa raia.
  • Baraza huru litakuwa na wanachama 11( watano wakiwa raia na watano watakuwa jeshi na mmoja atachaguliwa kulingana na makubaliano)
  • Waziri mkuu , atateuliwa na wanaharakati wa demokrasia na ataongoza baraza la mawaziri
  • Waziri wa ulinzi na mambo ya ndani atateuliwa na jeshi
  • Nafasi nyingine zitachukuliwa na wanaharakati wa demokrasia
  • Baraza huru na wajumbe wa baraza hawataruhusiwa kushiriki uchaguzi
Makubaliano hayo ya mpito yalionekana kama ushindi kwa wanaharakati wa demokrasia ingawa kipindi hiki cha mpito watu zaidi ya 120 tayari wameripotiwa kuuwawa na wengi kutupwa katika mto Nile

Post a Comment

0 Comments