Alexis Sanchez asema hajutii kujiunga na Man Utd

Alexis Sanchez

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAlexis Sanchez only started 31 of a possible 77 games while at Manchester United
Mshambuliaji Alexis Sanchez "hajutii" kujiunga na na klabu ya Manchester United lakini anasema hakupata muda wa kutosha wa kucheza na kuonesha makali yake.
Mchezaji huyo raia wa Chile, 30, amejiunga kwa mkopo na miamba ya soka nchini Italia, klabu ya Inter Milan, baada ya kudumu Old Trafford kwa miezi 19.
Sanchez alikuwa akilipwa mshahara mkubwa zaidi United wa pauni 400,000 kwa wiki - lakini amefunga magoli matano tu katika mechi 45 alizoichezea United toka alipoihama Arsenal Juanuari 2018.
"Ni furaha kwangu kuwa nilijiunga na Manchester United," Sanchez ameiambia BBC.
"Nimekuwa nikisema hivyo kila siku. Ni klabu iliyoshinda zaidi England.
"Nilipojiunga Arsenal ilikuwa ni jambo kubwa na zuri - Nilikuwa mwenye furaha pale (Arsenal) - lakini United ilikuwa ikitanuka, walikuwa wananua wachezaji ili kushinda kitu.
"Nilitaka kujiunga nao ili nami nishinde kila kitu."
Sanchez alipachika magoli 80 katika mechi 166 alizoichezea Arsenal ambao walimnyakua kutoka Barcelona kwa pauni milioni 30 Julai 2014.
Mwaka 2017, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi ya Primia.
Hata hivyo, kujiunga kwake na United kumeandamwa na kuporomoka kwa kiwango chake dimbani.
Alifunga magoli mawili tu katika mechi 27 za ligi alizocheza msimu uliopita. Japo aling'ara na timu ya taifa ya Chile kwenye kombe la Copa America akipachika magoli mawili nusu faiali.
Sanchez alianza kwenye michezo 31, kati ya 77 kwa United, na alimaliza michezo 13 tu.
"Naamini huwa na furaha sana ninapochezea timu yangu ya taifa," amesema.
"Nilikuwa mwenye furaha nikiwa na Manchester United pia, lakini nimekuwa nikiwaeleza rafiki zangu: nataka kucheza.
"Kama wataniruhusu kucheza nitafanya kila niwezalo. Wakati mwengine nacheza dakika 60 kisha mechi inayofuata sichezi, na sijui kwa nini."
Kabla ya kujiunga na Inter Milan, Sanchez hakucheza hata mchezo mmoja wa kirafiki wa kabla ya msimu na hakuwemo kwenye kikosi cha kocha Ole Gunnar Solskjaer kwenye michezo mitatu ya mwanzo huku klabu ikisema alikuwa majeruhi baada ya kuumia akiwa na timu ya taifa.
Hata hivyo, Sanchez anasema alikuwa tayari kuchezea klabu yake baada tu ya Copa America.
"Nilikuwa tayari na nimepona. Nilifanya vizuri. Baada ya hapo yalikuwa ni maamuzi ya kocha kunipanga nicheze. Inabini umuulize yeye (kwa nini hakupangwa) na si mimi."

Post a Comment

0 Comments