tangazo

Arsene Wenger ajuta kushindwa kumsajili Lionel MessiArsene Wenger anasema moja ya majuto yake makubwa akiwa kocha wa Arsenal ni kushindwa kumsajili Lionel Messi kutoka Barcelona.

Arsenal ilijaribu kumsajili Lionel Messi mwaka 2003 na kushindwa kuipata saini yake, Kipindi hicho ndipo walimsajili Cesc Fabregas.

“Tulikuwa tuna majadiliano na Messi kipindi tunamnunua Fabregas.” Wenger aliiambia beIN SPORTS .

Akaendelea kwa kusema, "Tulitamani kumsajili (Messi), lakini alikuwa hagusiki kwa kipindi kile” .
Messi anaungana na Cristiano Ronaldo katika moja ya wachezaji ambao Wenger alishindwa kuwasaini miaka ya nyuma akiwa kocha wa Arsenal".

Post a Comment

0 Comments