Brexit: Waziri Mkuu Boris Johnson akwaa kigingi bungeni


Boris Johnson 'aangukia pua' Bungeni Uingereza
Image captionBoris Johnson 'aangukia pua' Bungeni Uingereza
Wabunge walioasi kutoka chama tawala cha Conservatives pamoja na wale wa vyama vya upinzani wameishinda serikali ya Uingereza katika awamu ya kwanza ya kuzuia Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya (EU) bila ya mkataba.
Baada ya kupiga kura, wapinzania waliibuka na ushindi wa 328 dhidi ya 301 juu ya Bunge la Commons kuchukua udhibiti wa ajenda ya kujitoa EU, maarufu kama Brexit, hali inayomaanisha kuwa wabunge wanaweza kupeleka mswada wa kuchelewesha tarehe ya Uingereza kujitoa.
Waziri Mkuu Borriss Johnson amekuwa akiimarisha mipango yake ya kujitoa EU Oktoba 31, iwe kwa mkataba ama la, lakini mipango hiyo inapingwa vikali na wapinzani na baadhi ya wananchama wa chama chake cha Conservatives.
Baada ya kuangushwa Bungeni, Waziri Mkuu huyo amesema atatoa hoja ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu kabla ya wakati uliopangwa.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Jeremy Corbyn amesema muswada wa kupelekwa mbele tarehe ya Brexit unapaswa kupitishwa kabla ya nchi kwenda kwenye uchaguzi.
Kwa ujumla, wabunge 21 wa Conservatives, ikiwemo mawaziri wa zamani wa serikali walijiunga na vyama vya upinzani kuiangusha serikali yao.
Baada ya matokeo hayo, ofisi ya Waziri Mkuu, maarufu kama 10 Downing Street, imesema kuwa wabunge wote walioasi watafukuzwa kutoka kwenye chama.
Ofisi hiyo iliamini kuwa vitisho vya kuwafuta uanachama - na kufanyika uchaguzi - kungezima uasi ndani ya chama.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Jeremy CorbynHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKiongozi wa Kambi ya Upinzani Jeremy Corbyn amesema muswada wa kupelekwa mbele tarehe ya Brexit unapaswa kupitishwa kabla ya uchaguzi kufanyika.
Waziri Mkuu amesema muswada unaotakiwa na wa wabunge utaipa EU mamlaka ya majadiliano na hatimaye itasababisha "kutapatapa zaidi, kuchelewa zaidi na mvurugano zaidi".
Johnson akaliarifu Bunge kuwa hana namna nyengine zaidi ya kuendelea na mipango ya kuitisha uchaguzi mwezi Oktoba: "Raia wa nchi hii itabidi waamue."
Hii inamaana ya kuwa, wabunge sasa wana mamlaka ya kuendesha shughuli za Bunge na kuwawezesha kuandaa muswada utakaoungwa mkono na pande zote wa kumlazimisha waziri mkuu apeleke mbele tarehe ya kujitoa mpaka Januari 31, ama wabunge wakubali mkataba mpya, au wapige kura ya kuunga mkono kujitoa bila mkataba Oktoba 19.
BBC inafahamu kuwa serikali inataka kuitisha uchaguzi Oktoba 15, siku mbili kabla ya Mkutano Mkuu wa EU jijini Brussels, Ubelgiji.
Hata hivyo, ili hoja ya uchaguzi ipite, Bw Johnson atahitaji kuungwa mkono na cha ma kikuu cha upinzani cha Labour, sababu inabidi ipatikane theluthi mbili ya uungwaji mkono kati ya wabunge 650.
Tayari Bw Corbyn ambaye ndiye kiongozi wa Labour ameshatangaza kutaka muswada wa wabunge kwanza upitishwe ndio uchaguzi ufanyike ili "kuondoa uwezekano kabisa wa kujitoa bila ya mkataba".
BBC
Johnson na washauri wake wanaamini kuwa wengi miongoni mwa raia wa Uingereza wanamuunga mkono katika sera zake za Brexit, na kwenda kwenye uchaguzi kutakifanya chama chake kishinde kura na kuwa na mamlaka ya kuwasilisha matakwa ya wananchi.
Wapinzania pia wanaamini wataongeza wingi wao bungeni kwa kumpiku Waziri Mkuu na hatimaye kufanikisha Brexit ya mkataba.
Kalenda ya Brexit
Presentational grey line

Kuahirisha Bunge

wishoni mwa mwezi uliopita, Waziri Mkuu Boris Johnson aliomba ridhaa ya Malkia na kukubaliwa kusitishwa bunge kwa muda.
Hatua hiyo inatafsiriwa na wapinzani wake na wachambuzi huru kama mpango wa kulizuia bunge kuweka sauti kinzani juu ya mustakabali wa Brexit.
Waandamanaji
Image captionWaandamanaji katikati mwa London wakipinga kusitishwa kwa Bunge
Maandamano yameanyika kwenye pembe mabalimbali za Uingereza kupinga hatua hiyo, japo serikali inadai hatua hiyo si unyakuzi wa demokrasia.
Kilichotokea Bungeni kinadhihirisha wazi nguvu ya wabunge katika kupasisha ama kutibua mipango ya serikali juu suala hilo nyeti kwenye siasa za Uingereza na Ulaya.

Post a Comment

0 Comments