Burna Boy: 'Sikanyagi tena Afrika Kusini' asema msanii maarufu wa Nigeria


Burna BoyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBurna Boy
Msanii Burna Boy wa miondoko ya Afrobeat nchini Nigeria ameapa hatawahi kukanyaga Afrika Kusini baada ya ghasia dhidi ya raia wa kigeni kuzuka upya nchini humo.
Katika post kadhaa za Twitter masanii huyo wa miaka 28- alisema hajawahi kuzuru nchi hiyo tangu mwaka 2017 lakini hatawahi kurudi tena hadi serikali ya Afrika Kusini itakaposhughulikia suala hilo.
Lakini serikali inatakiwa ''kufanya miujiza ila sijui jinsi itakavyoweza kutatau suala hili", aliongeza.
Tayari polisi nchini Afrika Kusini imewakamata zaidi ya watu miamoja waliowashambulia raia wa kigeni katika miji ya Johannesburg, Pretoria na maeneo mengine.
Msanii huyo ambaye alishinda tuzo ya kimataifa ya BET mwezi Juni, amesema mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni yanaenda kinyume na maadili - na kugusia jinsi bara la Afrika lilivyoisaidia nchi hiyo katika mapambano dhidi ya utawala wa wazungu walio wachache.
"Naelewa miaka mateso waliopitia miaka mingi iliopita imewafanya Waafrika Kusini kuchanganyikiwa kiasi cha kuwachukulia kama maadui watu waliowasaidia wakati wa utawala wa kibaguzi," Burna Boy alianginda katika Twitter yake.
Aliongeza kuna raia wa Afrika Kusini ni ''watu wazuri na wapenda maendeleo "… lakini kwa hili wamepotoka".
Raia wa Nigeria waliojawa na ghadhabu walivamia na kuharibu mali katika duka la jumla linalolimikiwa na raia wa Afrika jatika mji wa kibiashara wa Lagos.
Waziri wa Nigeria wa Habari na Utamaduni Alhaji Lai Mohammed, ameelezea kusikitishwa kwake na ripoti kwamba Wanageria wameanza kuvamia kampuni za nchi hiyo zinazoendesha shughuli zake Nigeria.
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumanne Bw. Mohammed alisema hatua hiyo ni sawa na kujipiga mwenyewe.
''Wawekezaji wa MTN na Shoprite ni raia wa kigeni na wanaofanya kazi katika maduka hayo ni Wanigeria bila shaka kampuni hizo zikisitisha huduma zake kwa kuhofia kuvamiwa watakaoathirika ni watu wetu''aliongeza.
Alhaji Mohammed amewahakikishia Wanaigeria kuwa serikali inafanya kila iwezalo kukomesha mashambulio ya mara kwa mara dhi ya raia wake nchini Afrika Kusini.
Polisi wamepelekwa katika maeneo yote yaliokumbwa na vurugu na uporaji wa maduka huku sehemu zingine mali ya raia wa kigeni ikichomwa moto.
Wakenya pia ni miongoni mwa raia wa kigeni walioathiriwa na vurugu hizo. Balozi wa Kenya nchini Afrika Kusini Jean Kamau amethibitisha kuwa raia kadhaa wa nchi hiyo wameshambuliwa katika Mkoa wa Gauteng .
Watu 189 wamekamatwa kwa kujihusisha na ghasia, uharibifu wa mali na wizi katika maeneo tofauti tangu siku ya Jumapili.
Tamko la SADC
Jumuia ya Maendeleo Mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC, imelaani vikali matukio ya vurugu na mashambulio dhidi ya raia wa kigeni.
Katibu mkuu wa SADC DK Stergomena Tax amendika katika Twitter yake akitoa wito wa kufikiwa kwa suluhisho la kudumu kuhusu suala hilo.
Wasanii wengine wakosoa
Msanii Tiwa Savage wa Nigeria pia amefutilia mbali onesho lake katika tamasha la DSTV Delicious Festival litakaloandaliwa Johannesburg September 21 kama hatua ya kuelezea kughabishwa kwake na matukio ya yanaoendelea nchini Afrika Kusini.
Tiwa Savage ameandika katika Twitter yake kuwa hawezi kuvumilia vitendo vya kikatili vinanavyofanywa dhidi ya Wanigeria wenzake nchini Afrika Kusini.
Kwa upande wake mchekeshaji maarufu wa Afrika Kusini aliye na makao yake nchini Marekani Trevor Noah amewakosoa vikali wananchi wenzake kwa kuwashambulia wahamiaji wa kiafrika.
Katika kipindi chake cha Comedy Central, Trevor Noah alikosoa wimbi la vurugu linaloshuhudiwa katika maeneo tofauti humo kuwalenga raia wa kigeni.
"Wahamiaji wa kiafrika hawamiliki ardhi, hawaendeshi makampuni makubwa, hawamiliki kampuni za madini wala hawaendeshi kampuni za kuwinda wanyama pori katika maeneo maalum miongoni mwa vitu vingine," alisema Noah.
Msanii huyo aligusia kuwa kuna karibu wahamiaji milioni 2.3 wanaoishi nchini Afrika Kusini.
Wahamiaji hao wanajumuisha Waafrika, Wachina, Wabangladesh, Wahindi, Waarabu na Wazungu wa Ulaya waliozaliwa nchini Afrika Kusini.
Image captionTrevor Noah, Mchekeshaji maarufu wa Afrika Kusini aliye na makao yake nchini Marekani
Aliongeza kuwa kati ya wahamiaji hao milioni 2.3 Waafrika ni milioni 1.6 ambao wanaendesha biashara ndogo ndogo na kwamba haoni jinsi wanavyonyakua kazi za wenyeji.
Baadhi ya mataifa ya kiafrika yameeleza hofu juu ya raia wake dhidi ya chuki hiyo na kutoa tahadhari juu ya vurugu hizo.
Ubalozi wa Ethiopia nchini Afrika Kusini umewashauri raia wake walioko nchini humo kufunga maduka wakati wa vurugu hizo zikiwa zinaendelea katika mji wa kibiashara wa Johannesburg.
Vilevile wameshauriwa kuwa mbali na kutojihusisha na vurugu hizi vilevile kutotoka nje wakiwa wamevaa vito vya thamani.
Watu watano wameripotiwa kuuawa tangu ghasia hizo zilipozuka upya siku ya Jumapili.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na viongozi wengine wa Afrika wamelaani mashambulio hayo..
Kwa upande wake Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amemtuma mjumbe wake nchini Afrika Kusini "kuelezea kutoridhishwa kwake na jinsi raia wake wanavyo nyanyasika".Wakati huo huo waziri wa usafiishaji nchini Zambia, magari ya mizigo yasisafiri kuelekea Afrika kusini mpaka hali ya usalama itakapotengamaa.
Watu watano wameripotiwa kuuawa tangu ghasia hizo zilipozuka upya siku ya Jumapili.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na viongozi wengine wa Afrika wamelaani mashambulio hayo..
Kwa upande wake Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amemtuma mjumbe wake nchini Afrika Kusini "kuelezea kutoridhishwa kwake na jinsi raia wake wanavyo nyanyasika".Wakati huo huo waziri wa usafiishaji nchini Zambia, magari ya mizigo yasisafiri kuelekea Afrika kusini mpaka hali ya usalama itakapotengamaa.
Taarifa zinaripoti kuwa kuna malori kadhaa ya wageni yamekamatwa nchini humo huku magari mengine kadhaa yameripotiwa kuchomwa moto.
Shirikisho la Soka la Zambia limefutilia mbali mechi ya kirafiki kati ya Zambia na Afrika Kusini iliokuwa imepangiwa kuchezwa Jumamosi hii mjini, Lusaka.
Hatua hiyo inafuatia wimbi la mashambulio dhidi ya raia wa kigeni nchini humo.
Raia wa Zambia wamekua wakitumia mitandao ya kijamii kulishinikiza shirikisho hilo kufutilia mbali mechi kati ya Chipolopolo na Bafana Bafana kama ishara ya kupinga kinachoendelea.
Baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini wamelalamikia vurugu ambazo zinazoendelea nchini humo kuwa ni muendelezo wa chuki ya wenyeji dhidi ya raia wa kigeni.
Watanzania hao wamedai kuwa bado hali si shwari na inawawia vigumu wao hata kutoka nje kwenda maeneo ya mjini.
"Hali ni mbaya kwa kweli , usalama hamna" Yusuph Omar ameieleza BBC na kuongeza kuwa watu wanapigwa , wanachomwa moto na kuuawa.
Omar anasema kwamba hajui idadi kamili ya watu waliouwawa kutokana na vurugu hiyo lakini hali zao ziko matatani na wanaishi kwa hofu sana.
Ghasia dhidi ya wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika ni jambo ambalo si geni nchini Afrika Kusini, licha ya kulaaniwa na maafisa wa usalama na serikali ya nchi hiyo.
Kundi la wanaume ambao hawana ajira waliwashambulia wahamiaji kutoka Malawi wanaoishi katika mji wa Durban Afrika kusini mwishoni mwa mwezi Machi.
Ilifuata visa vingine kadhaa katika mji huo katika kipindi cha mwezi huo, jambo lililochangia viongozi kutoka vyama vitatu vikuu kushutumua mashambulio dhidi ya raia wa kigeni.

Post a Comment

0 Comments