tangazo

Familia ya Robert Mugabe yakasirishwa na mipango ya mazishi Zimbabwe 'inayokwenda kinyume na wosia wake'


The body of former Zimbabwean President Robert Mugabe arrives at the Blue Roof, his residence in Borrowdale, Harare, Zimbabwe, on 11 September 2019Haki miliki ya pichaREUTERS
Familia ya Robert Mugabe inasema imeshutushwa kwa kutoshauriwa na serikali kuhusu mipango ya mazishi ya aliyekuwa rais wa Zimbabwe.
Mugabe, alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 95, wakati akiwa anapokea matibabu katika hospitali moja huko Singapore.
Mwili wake unatayarishwa kulazwa ili kupewa heshima za mwisho kitaifa katika uwanja wa soka katika mji mkuu wa Zimbabawe, Harare.
Familia yake na serikali zinatofuatiana kuhusu sehemu atakapozikwa Mugabe.
Familia yake inasema mwili wake utalazwa kuonekana mara ya mwisho nyumbani kwake katika kijiji cha Kutama Jumapili usiku, na atazikwa katika mazishi ya faragha.
"Mwili wake utapewa heshima za mwisho Kutama Jumapili usiku na kufuatwa na mazishi ya faragha - pengine Jumatatu au Jumanne - na sio katika makaburila ya kitaifa ya mashujaa wa uhuru. Huo ni uamuzi wa familia nzima," binamu yake, Leo Mugabe ameliambia shirika la habari la AFP.
Rais Emmerson Mnangagwa alimtangaza Mugabe kuwa shujaa wa kitaifa baada ya kifo chake, na kuashiria kuwa anapaswa kuzikwa katika eneo hilo la kitaifa.
Enzi ya kisiasa ya Mugabe
Waziri wa elimu Paul Mavhima amesema hakuna shaka Mugabe anasathili kuzikwa kama shujaa wa kitaifa.
"Mtu muhimu wa aina hiyo, ambaye mazishi yake yatahudhuriwa na zaidi ya viongozi 50 wa taifa na wa zamani. Muasisi wa taifa hili hakupaswi kuwa na majadiliano ya hilo. hakupaswi kuwa na mzozo wowowte. Uamuzi unapaswa kuwa wa wazi, anastahili kuzikwa katika kaburi la kitaifa,"ameiambia BBC.
"Itakuwa ni makosa makubwa kuwa na mpiganiaji uhuru wa taifa hili, mhamasishaji mkubwa wa raia wa Zimbabwe kuzikwa katika eneo jingine lolote kando na kaburi la itaifa. Wito ni kuiomba familia - huyu sio wenu tena, ni kiongozi wa taifa. Ni kiongozi wa Afrika. Ni kiongozi duniani, Anastahili kupewa heshima anayoistahili . Kwahivyo atazikwa katika kaburi la kitaifa''
"Tumetambua na kwa wasiwasi mkubwa, namna serikali ya Zimbabwe ilivyoratibu mpango wa mazishi ya marehemu Robert Gabriel Mugabe pasi kuishauri familia yake marehemu ilio na jukumu la kuwasilisha maombi yake ya mwisho kuhusu mazishi yake," familia hiyo ilisema katika taarifa.
Mr Mugabe's body will be taken to his family home in HarareHaki miliki ya pichaREUTERS
" Kama familia yake ya karibu, tumetambua na kwa mshtuko kuwa serikali ya Zimbabwe inajaribu kutubembeleza tukubali ratiba ya mazishi ya marehemu Robert Gabriel Mugabe ambayo inakwenda kinyume na maombi yake ya kutaka mwili wake uhifadhiwe."
Taarifa hiyo inaongeza kuwa mojawapo ya maombi ya marehemu kiongozi huyo wa zamani ilikuwa ni kutaka mkewe, Grace Mugabe, asiondoke karibu na jeneza la Mugabe wakati wa mazishi mapaka atakapozikwa.
Familia ya Mugabe inasemekana kuwa na uchungu kwa namna Mugabe alivyotimuliwa na aliyekuwa mshirika wake Mnangagwa miaka miwili iliyopita.
Mugabe alimfuta kazi Mnangagwa mnamo 2017, katika kile ambacho wengi waliamini ni njia ya kumtayarisha Bi Mugabe kumrithi.
Mwili wa Mugabe baadaye ulipelekewa katika makaazi ya Mugabe mjini Harare yanayofahamika kama 'the Blue Roof' ambako familia na wafuasi wake walikusanyika kumuomboleza.
Mwili wa Mugabe utalaza katika uwanja wa michezo wa Rufaro Alhamisi kabla ya kuelekea katika makaazi yake ya Zvimba kwa misa ya wafu.
Mugabe alikuwa kiongozi wa kwanza wa Zimbabwe baada ya taifa hilo kupata uhuru mnamo 1980. Alishikilia madaraka kwa takriban miongo minne kabla ya kutimuliwa katika mapinduzi mnamo 2017.

Post a Comment

0 Comments