Israel na Hezbollah: 'Vita ambavyo havijatangazwa rasmi'


Israel and Hezbollah exchanged fire near the southern Lebanese town of Maroun al-RasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIsrael na Hezbollah zilikabiliana karibu na mji uliopo mpakani kuisni mwa Lebanon Maroun al-Ras
Mpambano wa hivi karibuni kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon huenda ukamalizika au la, lakini ishara zinaelekea kudhihirisha mzozo mkubwa na wenye maafa katika siku zijazo.
Pande zote zina maslahi katika kusitisha operesheni kwa sasa. Kila upande hautaki vita kamili . Itategemea pakubwa namna Hezbollah itakavyojibu mvutano huo ambao Israel ilijaribu kutuliza wimbi la hivi sasa.
Ni shambulio la Israel dhidi ya kituo cha Hezbollah cha Dahiya huko Beirut - kilichochangia makabiliano haya ya mpakani. Hili lilitazamwa na wachambuzi wa jeshi kama "ukiukaji wa sheria za mchezo".
Hili lilikuwa shambulio la kwanza la Israeli katika mji mkuu wa Lebanon tangu kuzuka vita baina ya Israel na Hezbollah mnamo 2006. Makabiliano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili kwa kawaida huwa ni nadra.

Israel inaaminika kulenga machine katika kiwanda iliyo muhimu katika utengenezaji wa propela za makombora na roketi. Hili linaonekana kama kulenga jitihada ya Iran kuimarisha shabaha na makombora tofauti yaliopo iliyowasilisha kwa washirika wake kieneo kama Hezbollah.
Shambulio hili lilitarajiwa kuchangia muitikio kutoka kwa Hezbollah na jeshi la Israeli lilijitayarisha vilivyo kwa kusogeza zana, kusitisha zoezi na kupunguza kiwango cha doria katika eneo la mpakani.
Hezbollah haikuchelea kujibu.
Israeli artillery unit near Israel-Lebanon border (01/09/19)Haki miliki ya pichaEPA
Image captionIsrael ilifyetua makombora 100 Lebanon kujibu shambulio la kombora
Makombora kidogo ya aina ya Kornet yalifyetulia katika ngome ya Israel na ambulensi iliohamiwa ikashambuliwa. Hezbollah ilikuwa mwepesi wa kudai ufanisi na kutangaza kuwa imeharibu gari la kijeshi katika kambi ya Avivim na kuwaua na kujeruhiwawaliokuwemo ndani."
Israel sasa inasema hakuna aliyejeruhiwa, lakini awali ilionekana kuidhinisha kilichoonekana kuwa uhamisho wa majeruhi kwa kutumia helikopta kama njia inayoonekana kuhumiza Hezbollah kuamini kuwa shambulio lake lilifanikiwa na hivyo kupata muda zaidi wa kudumisha utulivu.
Jibu la Israel kwa moto wa Kornet lilikuwani la kiasi fulani. helikopta ilishambulia eneo hilo ambalo lilikuwa ndio chanzo cha moto na makombora mengi yalifyetuliw na Israeli.
Je sasa kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah atahisi kuwa heshima ilitekelezwa au atataka kulipiza tena?
Mwandishi wa BBC wa masuala ya diplomasia Jonathan Marcus anatathmini kuwa hakuna ajuae ni kusubiria muda lakini pande zote hazitaki vita vishike kasi kwa sasa. Lakini Israeli ina maswali ya kujibu pia.
Smoke rises from shells fired from Israel in Maroun al-Ras villageHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMoshi unafukuta katika kijiji cha Maroun al-Ras nchini Israel
Marcus anaendelea kuchambua kuwa watapatiliza fursa katika siku zijazo kuushambulia mpango wa Hezbollah unaoungwa mkono na Iran huko Lebanon wakitambua fika kuwa ni kukiuka zinazotajwa kuwa "sheria za mchezo"?
Ama kwa hakika huu sio mchezo, na 'sheria' ni za muda.
Kinachoendelea hapa ni vita ambavyo havijatangazwa sio tu baina ya Israel na Hezbollah, lakini pia baina ya Israel na mfadhili wa Hezbollah, Iran.
Kwa tafisri ya kijiografia, vita hivi ni vikubwa kuanzia Lebanon na kuzama ndani ya Syria. Huenda pia maeneo ndani ya Iraq yamelengwa kwa makombora ya Israeli.
BBC map
Presentational white space
Iran inajaribu kupiga hatua katika maeneo matatu. Kwanza inataka kuendelea kutoa makombora kwa washirika wake kieneo.
Pili inataka kuendelea kulisaidia Hezbollah kuimarisha uwezo wa makombora ambayo inamiliki tayari.
Na tatu inatafuta kupatiliza ushawishi ilio nao kutokana na kuungw mkono utawala wa Assad nchini Syria, ili iweze kujikita huko kama mshawishi wa kijeshi kwa kiasi fulani kufungua fursa mpya dhidi ya Israel.
Israel imeendelea kuishambulia Iran na hivi karibuni imesema iliharibu shambulio la ndege isiyokuwa na rubani ya Iran ndani ya Israel.
United Nations peacekeeping forces patrol a road near the Israeli-Lebanese borderHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Washirika wa nje wanaonekana hawawezi kubadili muelekeo wa Tehran.
Ni wazi kuwa Marekani haipo katika nafasi ya kufanya hivyo. Na hakikisho la Moscow kuwa iwaishawishi Syria kuzuia ushawishi wa Iran limeonekana kuambiliwa patupu, anaeleza mwandishi wa BBC wa masuala ya kidiplomasia Marcus.
Mashambulio ya angani ya Israeli yanaonekana kuongezeka kasi baada ya mkutano wa Juni katiya washauri wa usalama wa kitiafa wa Israel , Urusi na Marekani.
Kwahivyo makabiliano katika vita hivi ambavyo havijatangazwa huenda vimemalizika, lakini mapambano yanaendelea. Na hatari ya kushika kazi au kuongezeka inaonekana kukaribia.

Post a Comment

0 Comments