tangazo

Je, siri gani zinafichwa katika 'safe house' za Uganda?

geti

Juhudi za kamati ya bunge ya haki za binadamu nchini Uganda kuzuru sehemu kunakodaiwa watu huzuiliwa kinyume na sheria zimegonga mwamba mara baada ya kuzuiliwa na idara ya usalama ya ISO.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya haki za binadamu Bi. Natume Engunyu amefahamisha jinsi walivyozuyiwa katika nyumba za safe house zinazotumiwa na vikosi vya ujasusi.
"Mkuu wa sehemu hii ametwambia twende tupate ruhusa kwa mkurugenzi wa Idara ya usalama wa nchini ISO, yeye ndiye mkuu wa sehemu hii.
Hi ni habari za kusikitisha, kama vitu vinavyotendeka hapa ni vizuri hakuna sababu ya kutuzuia kuingia.
Sisi kama kamati tunarudi bungeni kuamua tutakachofanya" Bi. Natume alifafanua.
Sehemu hizo maarufa kama 'safe houses' zilithibitishwa kuwepo na waziri wa usalama wa ndani wiki jana na naibu spika wa bunge akaagiza wabunge kwenda huko kuthibitisha madai ya watu kuteswa.
Waziri huyo wa usalama Jenerali Elly Tumwine alikiri kuepo kwa nyumba hizo na kudai kuwa huwa zinazotumiwa kwa njia ya kiintelijensia, "Hata mimi mwenyewe siwezi kufahamu ni nyumba ngapi zinazotumiwa na vikosi vyote vya ujasusi nchini Uganda.
Nyumba za safe house zipo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa siri na hivyo haziwezi kufahamiki, zipo kwa ajili ya kupata maelezo ya kina, upelelezi haufanywi hadharani, upelelezi unafanywa kwa siri hivyo unawaita watu sehemu ya siri , na kuanza kufanya upelelezi zipo kwa kupata maelezo ya siri na maelezo ya faida, na huwa wanafahamishwa,"Elly Tumwine alifafanua wiki mbili zilizopita.
kamati
Mmoja wahadhiriwa wa mateso katika Safe house ni Dk.Ismail Kalule ambaye amekamatwa mara sita na kupelekwa nyumba hizo za mateso anakanusha maneno ya waziri miaka 11 iliyopita.
Kalule anasema kuwa aliwahi kupelekwa katika nyumba hizo na aliteswa.
Mbunge Latifu ssebagara aliyepeleka hoja hiyo bungeni amesema licha ya kuzuiwa wataendelea kupambana kuona haki inatendeka kwa watu wanaonyanayaswa katika safe house.
Mkurungezi mkuu wa Idara ya usalama wa nchini humo anatarajiwa kufika katika kamati hiyo ya haki za bindamu na wajumbe wanamsubiri kumuuliza kwanini wamezuiliwa kuingia safe House.
k
Miongoni mwa wajumbe katika kamati hiyo ni pamoja na mbunge msanii maarufu Bobi Wine anaelezea masikitiko yake baada ya kuzuiwa.
"Hii inaonyesha kwamba hakuna sheria nchini Uganda tunaruhusiwa kisheria kutetea haki za binaadamu lakini tumezuiliwa kuingia ndani" Bobi Wine alieleza.
ug
Vikundi vya kutetea haki za binadamu siku za nyuma ziliwahi kuhoji serikali juu ya nyumba hizo za siri zinazowashikilia watuhumiwa.

SOURCE: bbc swahili

Post a Comment

0 Comments