tangazo

Kipa afariki akiwa kwenye kambi ya timu ya taifaKipa wa timu ya taifa ya Curacao Jairzinho Pieter amefariki dunia  akiwa katika kambi ya timu yake ya taifa wakati ambao ilikuwa ikijiandaa na mchezo dhidi Haiti.

Jairzinho ,31, alikuwa sehemu ya Kikosi cha Curacao kinachojiandaa mchezo wa CONCACAF Nations League dhidi ya Haiti.

Shirikisho la soka la taifa lake limeeleza kuwa Jairzinho amefariki akiwa katika hoteli ya Port-au-Prince, nchini Haiti ilipokuwa imeweka kambi timu yake ya taifa.

Waziri wa michezo wa Curacao Edwing Charles amethibitisha kuwa chanzo cha kifo cha kipa huyo wa akiba wa timu hiyo ni tatizo la moyo ambalo alikuwa nalo

Licha ya kifo hicho wachezaji Curacao walisisitiza mechi yao na Haiti ichezwe ili kutoa heshima kwa kipa wao. Mechi hiyo ilichezwa usiku wa kuamkia jana na kuisha kwa sare ya 1-1.

Post a Comment

0 Comments