Kwa nini shirika la ujasusi la Marekani CIA halikugundua shambulio la Septemba 11 lililolenga majengo 2 ya New York


Mashambulizi ya Septemba 11 yameonekana kama kufeli kwa CIAHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kufeli kwa shirika la ujasusi nchini Marekani CIA kugundua ishara na onyo la shambulio la Septemba 11 2001 , limekuwa mojawapo ya maswala tata katika historia ya huduma hiyo ya ujasusi.
Kumekuwa na tume, hakiki, uchunguzi wa ndani na zaidi. Upande mmoja kuna wale wanaosema kwamba CIA hawakuziona ishara za mapema.
Kwengine kuna wale wanaosema kwamba ni vigumu sana kugundua vitisho mapema na kwamba kitengo hicho cha ujasusi nchini Marekani kilitumia kila njia.
Je ni nini kitakachotokea iwapo pande zote mbili zina makosa?
Je inakuwaje iwapo sababu ya CIA kufeli kugundua shambulio hilo ipo wazi zaidi ya watu wanavyodhania?
Na itakuwaje iwapo nitakuambia kwamba shida hii imesambaa zaidi ya huduma za Ujasusi na inaathiri maelfu ya mashirika, serikali na makundi hii leo?
Huku uchunguzi mwingi ukiangazia kile ambacho shirika hilo lilifanya ama kushindwa kufanyia habari ilizokuwa nazo kabla ya shambulio la 9/11, watu wachache walirudi nyuma na kuchunguza jinsi shirika hilo lilivyoundwa na hususan sera yake ya kuajiri.
Na kwa mtazamo wa jadi, hawakuweza kuhimili: Wachambuzi walikabiliwa na majaribio ya kisaikolojia, ya matibabu na ya kila aina. Na bila shaka waliajiri wataalam.
"Mitihani mikuu miwili ilikuwa ile inayolinganishwa na mtu anapojiunga na chuo kikuu ambayo inabaini intelijensia ya anayeomba kazi mbali na wasifu wa kisaikolojia kuchunguza hali yake ya kiakili," anafafanua mfanya kazi wa zamani wa CIA
"Vipimo hivyo viliwaondoa watu ambao hawakuwa bora katika kesi zote mbili.
Katika mwaka niliowasilisha maombi yangu, nilikubali muomba kazi kwa kila waombaji 20,000. Wakati CIA ilisema iliajiri watu bora, ilikuwa nyongeza sawa.
Na wengi ya walioteuliwa pia walikuwa wakifanana: Wanaume, weupe, Wamarekani, watu wa dini ya Protestant.
Hili ni swala la kawaida katika kuajiri watu. Watu huajiri watu wanaojiona kuwa wenyewe.
Wakati wa Shambulio hilo wachanganuzi wenginwa CIA walikuwa na fikra sawaHaki miliki ya pichaAFP
Katika utafiti wao wa CIA, mtaalam wa Kiintelijensia Milo Jones na Phillipe Silberzahn waliandika: Sifa ya utambulisho wa kitengo cha CIA na utamaduni kuanzia 1947 hadi 2001 ni mchanganyiko wake wa wafanyakazi wake kutokana na rangi, jinsia, kabila na tabaka kihistoria.
Na utafiti uliofanywa na inspekta jenerali kuhusu kuajiri ulibaini kwamba 1964 , tawi la CIA , na idara za takwimu za kitaifa haikuwa na wataalama weusi , Wayahudi , wanawake na kwamba ilikuwa na wafuasi wachache wa kanisa la Katoliki.
Kufikia mwaka 1967 , kujlingana na ripoti , kulikuwa na wafanyakazi 20 wenye asili ya Wamarekani weusi kati ya wafanyakazi 20,000 huku idara hiyo ikiendelea na utamaduni wake wa kutowaajiri watu wa kundi la walio wachache kutoka 1960 hadi 1980.
Na hadi 1975, jamii ya kiintelijnsia ya Marekani , waziwazi ilipinga kuajiriwa kwa wapenzi wa jinsia moja.
Akizungumza kuhusu uzoefu wake na shirika la CIA 1980, mtu aliyekuwa na habari za ndani aliandika kwamba mchakato wa kuajiri ulisababisha kuonekana kwamba wale walioajiriwa wanafana na wale waliokuwa tayari washaajiriwa wakiwemo watu weupe, watu wa tabaka la katikati , matajiri , wale wanotoka katika vyuo vikuu.
Ulikuwa na wanawake wachache , makabila machache kutoka Ulaya. Mchanganyiko huo ulipungua zaidi baada ya vita vya dunia.
Makao makuu ya CIA langley VirginiaHaki miliki ya pichaAFP
Afisa mmoja alinukuliwa akisema CIA ina maafisa wanaofana kama mchele. Na miezi kadhaa kabla ya shambulio la Septemba 11, jarida la kimataifa kuhusu Intelijensia liliandika: Tangu kuanzishwa kwake, jamii ya Ujasusi ilishirikisha watu weupe sio kwamba ndio lililokuwa tabaka katika uongozi bali kwa sababu walionekana kama wadhamini na walinzi wa maadili na thamani ya Wamarekani.
Lakini ni kwa nini swala hili la ajira katika kitengo hicho ni tatizo? Unapounda kikosi cha wanariadha cha mbio za kupokezana vijiti, unatazama wanariadha wenye kasi.
Kwa nini ni muhimu iwapo wana rangi ya kufanana, jinsia ama hata tabaka? Kwa sababu wakati kuna tatizo kuu hakuna mtu aliye na majibu yote, kila mtu ana dosari yake.
Na iwapo mtu ataajiri kundi la watu wanaotoka katika eneo moja kuna uwezekano mkubwa kwamba watatoa suluhu inayofanana wakati wa tatizo.
Osama Bin Laden alitangaza vita dhidi ya Marekani kutoka katika pango moja eneo la Tora Bora mnamo mwezi Februari 1996.
Picha zilimuonyesha mtu aliyekuwa na ndevu zilizokuwa zimefika chini ya kifua chake.
Alikuwa amevalia Joho ndani ya sare ya kijeshi aliyovaa. Hii leo, baada ya kujua kila kitu kilichofanyika tamko lake linaonekana kuwa la kutisha.
Lakini chanzo kutoka kwa Idara ya ujasusi ya Marekani CIA kilisema kwamba hakiamini kwamba mtu huyo alie na ndevu anaweza kuwa tishio la Marekani.
Osama bin Laden alitangaza vita dhidi ya Marekani kutoka katika pango nchini Afghanistan mnamo mwezi Okotba 1998Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Upande mwengine ni kwamba hakuna uchanganuzi wowote aliodhani kwamba Bin laden anaweza kuwa tishio.
Mwengine alisema: Hawakuweza kufadhili uchunguzi wowote ili kujua zaidi kuhusu Bin Laden na Al Qaeda kwa kuwa mtu huyo alikuwa akiishi pangoni.
Kwao alikuwa mtu ambaye alipitwa na wakati.
Richard Holbroke afisa mwandamizi katika utawala wa rais Clinton alisema Inawezaje mtu anayeishi pangoni kuwashinda viongozi katika jamii ya habari? sasa fikiria mtu kutoka jamii ya Waislamu ambavyo angezichukulia picha za Osama.
Bin Laden alivalia joho sio kwa sababu alikuwa amgtu aliyepitwa na wakati asiye na fikra nzuri ama asiyejua teknolojia, bali kwa sababu alitaka kufanana na mtume Muhammad.
Alifunga siku kama zile ambazo mtume Muhammad alifunga. Mienendo yake ambayo ilionekana kama mtu aliyepitwa na wakati kwa jamii ya magharibi ilifanana na tamaduni za Kiislamu zilizotokana na mitume yao.
Kama Lawrence Wright anavyoelezea katika kitabu chake Septemba 11 ambacho kilimshindia tuzo la Pulitzer kwamba Bin laden alitekeleza Operesheni zake akitoa picha ambazo zilikuwa na maana ya ndani kwa Waislamu wengi lakini hazikueleweka miongoni mwa wale ambao hawakuwa Waislamu.
Wachanganuzi wa CIA hawakuona tishio lililokuwa likiwakabiliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Sasa fikiria mtu anayeijua dini ya Kiislamu jinsi ambavyo angepokea picha hizo.
Kuhusu pango alilokuwa akijificha ..lina maana ya undani zaidi.
Kama vile kila Muislamu anavyojua , Mtume Muhammad alitafuta hifadhi katika pango baada ya kuwatoroka waliokuwa wakimtafuta Mecca. Kwa Waislamu pango ni eneo takatifu .
Na Bin laden alitumia maficho yake huko Tora Bora kama Hajj yake akitumia pango hilo kama propaganda.
Kama msomi mmoja wa Kiislamu alivyosema: Bin Laden hakuwa mjinga , alikuwa mtu wa mkakati. Alijua jinsi ya kutumia Quran kuwashawishi wale ambao baadaye wangekuja kuwa mashahid katika shambulio la Septemba 11.
Wachanganuzi pia walidanganywa kwamba bin Laden alikuwa akitoa taraifa zake kupitia mashairi.
Kwa wazungu wenye tabaka la katikati alionekana kama Mullah aliyepitwa na wakati kwa kuishi katika pango.
Hatahivyo kwa Waislamu ushairi una maana tofauti kwani ni njia nzuri ya kuwasilisha ujumbe na kundi kama vile Taliban limekuwa ikitumia mbinu hiyo kuwasilisha ujumbe wake.
Hatahivyo kitengo hicho cha Marekani kilikuwa kikichunguza matamshi ya Bin laden kikitumia ulinganishaji.
Bin laden alijua jinsi ya kuitumia Koran kuwachochea wale ambao wanegkuwa mshahidi katika shambulio hilo la Sepetmba 11Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kufikia mwaka 2000 ufuasi wa Bin laden ulikuwa umefikia watu 20,000 wengi wao wakiwa na elimu ya taasisi na kupendelea uhandisi.
Yazid Sufaat ambaye alikuwa mtafiti mkuu wa kundi la Al Qaeda alikuwa na shahada katika somo la kemistry . Na wengi walikuwa tayari kuuawa kwa dini yao.
Wakati huohuo , afisa mwandamizi Paul Pillar hakufikiria kwamba kuna uwezekano wa shambulio kubwa la kigaidi kufanyika.
Na dosari jingine la CIA ilikuwa kuchelewa kwake kuamini kwamba Bin laden ataanzisha mgogoro na Marekani.
Kwa nini nianze vita ambavyo sitashinda?
wakati marekani ilipogundua hatari inayotokana na Bin Laden walikuwa wamechelewa.Haki miliki ya pichaAFP
Wachanganuzi hawakuelewa kwamba watu wanopigana vita vya Jihad , ushindi haufai kuhakikishwa duniani bali peponi.
Ukweli ni kwamba Mpango huo wa Al-Qaeda uliitwa ''Harusi kuu''.
Na ni itikadi ya watu wanaojitoa muhanga , kwamba siku ya kifo cha muuaji pia ni siku ya harusi yake, wakati anapokelewa na mabikira mbinguni.
CIA ingeongeza ufadhili wake kulichunguza kundi la Al- Qaeda. Ningejaribu kuingia ndani ya kundi hilo. Lakini katika shirika hilo la kijasusi hawakuona sababu muhimu ya kufanya hivyo kwa haraka.
Hawakuongeza ufadhili kwa sababu hawakuona tishio.
Ukosefu wa Waislamu katika shirika hilo la CIA ni mojawapo ya mifano ya jinsi ukosefu wa watu wa jamii tofauti ulivyodhoofisha kitengo hicho cha ujasusi kinachoongoza duniani, na inatoa wazo la jinsi watu kutoka jamii tofauti wangeweza kutoa suluhu ya tishio kama hilo la al-Qaeda.
Lakini tatizo sio CIA pekee kwa kuwa unapotazama mabaraza ya mawaziri, kampuni za mawakili, uongozi wa kijeshi, na maafisa waandamizi pamoja na maafisa watendaji katika makampuni ya kiteknolijia pia tatizo hilo linapatikana.
Katika kundi la wafanyakazi kutoka sehemu tofauti kila mmojawao angekuwa na mchango tofauti kuhusu tishio hiloHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Waajiri huwapendelea watu wanofanana nao hivyobasi tunashindwa kuona hatari kwa sababu hatujui dosari zetu.
Hatahivyo Shirika la Ujasusi la CIA limechukua hatua muhimu la kuorodhesha watu kutoka maneo tofauti miongoni mwa wafanyakazi wake tangu shambulio hilo la Septemba 11 kufanyika.
Lakini tatizo hilo linaendelea kulikabilia shirika hilo na ripoti ya ndani kwa ndani ya mwaka 2015 ilitoa ukosoaji mkubwa.

Post a Comment

0 Comments