tangazo

Maamuzi ya Kocha wa Man United yaanza kukosolewa


Uamuzi wa kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer wa kugawa sawa majukumu ya kupiga mikwaju ya penalti kikosini mwake, umetajwa kuwa ni mambo ya kitoto na nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Matt Le Tissier.

Man United ilikosa penalti mfululizo katika mechi dhidi ya Wolves na Crystal Palace mapema msimu huu baada ya Paul Pogba na Marcus Rashford kushindwa kufunga mikwaju ya penalti.

Kutokana na kukosa huko, Solskjaer alilazimika kufafanua kuwa wawili hao wataamua wenyewe nani apige penalti msimu huu, hali ambayo Le Tissier anaona ni udhaifu mkubwa wa kiuongozi.

Post a Comment

0 Comments