tangazo

Mahakama ya juu ya Marekani yampa Trump idhini ya kukabiliana na wahamiaji


Migrants in El Paso, TexasHaki miliki ya pichaREUTERS

Mahakama ya juu zaidi nchini marekani imeupatia idhini utawala wa Trump kuendelea na mipango yake inayopunguza uwezekano wa wahamiaji a kuomba ukimbizi nchini Marekani.
Kulingana na sheria hiyo , watu watakaokuwa wakiwasili nchini Marekni watatakiwa kuomba ukimbizi kabla ya kufika kwenye mpaka wa Marekani.
Upinzani wa kisheria dhidi ya uamuzi huo wa mahakama bado unaendelea , lakini uamuzi huo unamaanisha kuwa kwa sasa inaweza kutekelezwa kote nchini Marekani.
Rais Donald Tametma ujumbe wake wa Twitter akisema uamuzi huo ni "Ushindi MKUBWA wa mahakama ya ngazi ya juu ya Marekani !".
Kukabiliana na uhamiaji kwa Marekani limekuwa ni lengo kuu la rais wa Marekani na moja ya malengo yake makuu aliyoazimia kuyatumia katika kampeni za kuwania kiti hicho tena mwaka 2020.
Wakati ilipofichuliwa mapema mwezi Julai sheria hilo nusura izuwiwe kutekelezwa , kwa hiyo hatua ya sasa ya Mahakama inaangaliwa kama ushindi kwa utawala wa Trump kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Mabadiliko ya sheria yana maana gani ?
Wahamiaji kutoka Amerika ya kati ambao kwa kawaida husafiri kwa miguu kupitia Mexico hadi wanafika kwenye mpaka wa Marekani. Weng wa wale wanaowasili huwa ni wale wanaotoroka ghasia au Umaskini.
Mabadiliko ya sheria yanamaana kuwa wahamiaji kutoka Honduras, Nicaragua na El Salvador mwatatakiwa kuomba ukimbizi katika nchi jirani au Mexico. Lakini sheria hii inawaathiri watu kutoka nje ya kanda hiyo pia wanaotaka ukimbizi nchini Marekani.The Africans risking death in the jungle trying to reach the US

Muungano unaopigania uhuru wa kiraia wa Marekani , uliopinga uamuzi wa mahakama , ulidai kuwa inawanyima uhuru watu wanaopaswa kupewa ukimbizi.
"Marufuku iliyowekwa sasa hatimae itawazuwia kabisa watu kuomba ukimbizi kutoka kwenye mpaka wa kusini , hata katika vituo vya mipaka ya kuingia nchini, kwa kila mtu isipokuwa Wamexico ," ulisema waraka wao kw amahakama wa kupinga sheria mpya.
Yeyote ambaye atakataliwa na nchi ya tatu alikoombea ukimbizi au muathiriwa wa biashara haramu ya binadamu bado anaweza kuiomba hifadhi ya ukimbizi.

Central America map

Ni kwa nini sheria hii ina utata?
Sera hiyo imegeuza utamaduni wa kawaida wa Marekani ambayo imekuwa ikisikiliza madai ya wahamiaji wanapofika mpakani.
Jaji Ruth Bader Ginsburg na Sonia Sotomayor walipinga sheria hiyo miongoni mwa majaji tisa wa mahakama ya juu ya Marekani

Migrants near the US port of entry at the Gateway International Bridge in Matamoros, Tamaulipas, Mexico, 24 AugustHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWahamiaji katika mpaka mwezi uliopita katika maeneo ya Matamoros, Tamaulipas, nchini Mexico

Barabara ya kuelekea Marekani ni hatari , huku wahamiaji wa Ameika ya kati mara nyingi wakikabiliwa na uwezekano wa kushambuliwa na magenge ya wahalifu katika nchi jirani na Marekani .
Kuna swali juu ya ikiwa Mexico na Guatemalazinaweza kumudu wimbi la wahamiaji wanaotaka kuingia nchini Marekani .
Mexico mara kwa mara imekataa pia kuwa nchi inayowapokea wahamiaji wanaotaka kuingia Marekani " Kuwa nchi ya tatu ya mhamiaji " ina maanisha kwamba italazimika kuchunguza madai ya wahamiaji wanaotaka kuingia nchini Marekani.

Post a Comment

0 Comments