tangazo

Mechi za leo kufuzu Kombe la Dunia 2022 Qatar


Baada ya timu kadhaa kufanikiwa kuingia hatua ya makundi baada ya kushinda mechi zake za marudiano zilizopigwa wikiendi iliyopita, leo viwanja kadhaa vitashuhudia vumbi zikitimka kwa mechi kadhaa kupigwa.

Malawi watakutana na Botswana, ambapo Eswatini wao watamenyana na Djibouti, Zimbabwe watavaana na Somalia, huku Msumbiji watakutana na Mauritius.

Kwa upande wao Angola watakipiga na Gambia, Togo na Comoro, Guinea Bissau watakipiga na Sao Tome e Principe, Rwanda na Shelisheli, huku Namibia uso kwa uso na Eritrea, na Sudan watamenyana na Chad.

Post a Comment

0 Comments