tangazo

Mwili wa Robert Mugabe kuwasili Zimbabwe leo kutoka Singapole kwa mazishi

Robert Mugabe

Image captionRobert Mugabe
Mwili wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe aliyefariki dunia Ijumaa unasafirishwa leo kurejeshwa nyumbani kutoka Singapore kwa ajili ya mazishi.
Bwana Mugabe ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 , alikuwa hospitalini kwa matibabu nchini Singapore. Awali serikali imethibitishwa kuwa mazishi yake yatafanyika katika siku mbili za wikendi ijayo
Taratibu za kitaifa za kuuaga mwili wake zitafanyika siku ya Jumamosi , kabla ya kuzikwa kijijini kwao Jumapili.
Robert Mugabe, ambaye alikuwa kiongozi wa vita vya msituni ambaye aliiongoza Zimbabwe baada ya Uhuru mwaka 1980, aling'olewa madarakani kma raia mwaka 2017.
Bwana Mugabe alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95, akiwa hospitalini Singapore wiki iliyopita.
Mugabe ambaye anakumbukwa na wengi kama mkombozi ambaye aliwaondoa watu wake katika pingu za ukoloni wa wazungu walio wachache anakumbukwa na wengine kama mtu aliyeangusha uchumi wa moja ya chumi zilizotazamiwa kufanya vizuri zaid barani Afrika na ambaye aliwatesa kikatili wapinzani wake.
Awali kulikuwa na utata kuhusu ni wapi atakapozikwa huku ambapo baadhi ya ndugu zake walitaka azikwe katika kijijini alikozaliwa cha Kutama kilichopo katika jimbo la magharibi la Mashonaland yapata kilomita 80 au maili 50 magharibi mwa mji mkuu Harare.
Familia ya Mugabe inapinga mpango wa serikali wa kumzika katika makaburi ya mashujaa wa taifa katika mji mkuu wa Zimbabwe -Harare na wanataka azikwekwe katika kijiji alikozaliwa.
Wengi miongoni mwa mashujaa wa taifa la Zimbabwe - wale ambao walishirikiana katika mapambano dhidi ya utawala wa wazungu walio wachache wamezikwa katika eneo la makaburi ya Mashujaa lililopo nje kidogo tu ya mji mkuu Harare.
Unaweza pia kutazama:
Enzi ya kisiasa ya Mugabe

Post a Comment

0 Comments