Naibu Waziri wa Madini atoa agizo kwa Maafisa Madini nchini



Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameagiza maafisa Madini nchini (RMO) kuhakikisha mialo yote inayoosha udongo wa dhahabu inasajiliwa na kutambulika ikiwemo kusimamiwa.

Aliyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara yake wilaya ya Chunya mkoani Mbeya ambapo alisema pia suala la uchomaji wa dhahabu usifanyike kiholela ichomwe sehemu moja japo kuna changamoto maeneo mengine inakuwa vigumu.

Alisema maafisa hao wanapaswa kuweka maeneo yanayofahamika ya kufanya uchenjua lakini wakati wa kuchoma waende sehemu moja huku akieleza kwamba wanafanya hivyo kwa sababu dhahabu ya mecury bado inapotea .

“Mnafanya vizuri sana lakini kuna baadhi yetu bado wapo miaka ya nyuma wanafikiria kutorosha dhahabu…mnafahamu uchenjuaji wa dhahabu asilimia 30 ya dhahabu inapatikana inayobaki inakwenda kuchenjuliwa kwenye Vatirichingi”Alisema

“Lakini niwaambia kwamba bado sijaridhishwa na dhahabu inayoonekana kwenye mecury kutokana na kwamba bado inapitishwa njia za panya wataalamu wetu wanaona kilo 20 tu kwa mwezi lakini sasa hivi tunaona kilo 120 “Alisema

Naibu Waziri huyo alisema kwamba hivi sasa wameanza operesheni maalumu kanda ya ziwa na maeneo mengine kudhibiti dhahabu ya mercury iende kwenye soko.

“Nikasema ujumbe wana chunya wangu nikuwaeleza mabroka na madila hakikishani mnanunua dhahabu na iwekeni kwenye soko kuna watu maeneo mengine unakuta dhahabu bei ya gramu ni sh.elf 96000 ukileta kwenye soko utakatwa asilimia 7 hivyo unaona fedha zitapungua atapotokea mnanuzi mwengine pembeni anakuambia atakupa elfu 95 usipeleka kwenye soko wewe unakubaliana naye unamuuzia “Alisema

Hata hivyo alieleza kwamba lazima wachimbaji watambue kwamba hiyo dhahabu wanayochimba ni mali ya serikali na wamepewa leseni ya uchimbaji kwa niaba ya serikali hivyo wakisha chimba kwa gharama zako zirudishe lipa mrabaha wa serikali baki na faida yako upeleke nyumbani ukikwenpa kodi unakuwa adui namba moja kwa sababu unainyima serikali mapato ambayo yangeweza kuwaaid kusukuma gurudumu la maendeleo.

Post a Comment

0 Comments