tangazo

Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Afrika


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Afrika kuhusu Rushwa ikiwa ni ziara ya Bodi hiyo kutathmini utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Afrika dhidi ya Rushwa. Bodi hiyo umeongozwa na Bw. Miarom Begoto.

Tanzania ni mwenyeji wa Bodi hiyo kupitia Mkataba wa Uenyeji kati yake na Umoja wa Afrika ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni mratibu mkuu na msimamizi wa utekelezaji wa shughuli za Bodi. Mazungumzo hayo yanefanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.Post a Comment

0 Comments