Rais Magufuli ataka vijana wasaidiwe kuchagua wenza wanaowataka


Rais John MagufuliHaki miliki ya pichaEMPICS
Image caption''Nimeambiwa siku hizi wanawake wanawatolea mahali wanaume'',amesema rais Magufuli
Watendaji kata wametakiwa kuwasimamia vijana ili wapate ajira na kuweza kujikimu kimaisha na kuweza kutoa mahali. Rais Magufuli amezungumza hayo katika mkutano na watendaji wa kata.
''Nimeambiwa siku hizi wanawake wanawatolea mahali wanaume''.
Amesema kuwa watendaji wa kata ndio wenye jukumu la kuwasimamia vijana katika kata zao, kwa kuwadhamini kwa saini zao wanapohitaji kujiendeleza kwa shughuli zao.
''Vijana hao wakifanya kazi mbaya athari yake itakuwa ni kubwa, ila akifanikiwa basi ataweza hata kujenga nyumba kubwa... hata kama atakuwa hajaoa ataoa mwanamke anayemtaka...
Siku hizi nasikia wanawake wanawatotea mahali wanaume...nasema uongo jamani?, nasema uongo akina mama?...
Inawezekana siku hizi ukimpenda mwanamke na huna hela ya kumtolea mahali basi anajitolea mwenyewe...Na ndio maana naambia vijana wa siku hizi wanapenda wanawake wenye magari..
.Aah...huo ndio ukweli , ili kusudi mwanamama akienda kazini yeye awe anaendesha hilo gari .
Kwa hiyo inawezekana watendaji wa kata akinamama wenye magari wana vijana huko wanacheza nao''. Amesema Magufuli huku hotuba yake ikikatizwa na kicheko cha watendaji wa kata.
Mnamo mwaka 2017 Rais wa Tanzania John Magufuli alisema kuwa chini ya uongozi wake wasichana wa shule ambao hujifungua watoto hawataruhusiwa tena kurudi shuleni
Image captionMnamo mwaka 2017 Rais wa Tanzania John Magufuli alisema kuwa chini ya uongozi wake wasichana wa shule ambao hujifungua watoto hawataruhusiwa tena kurudi shuleni

Hii si mara ya kwanza kwa rais wa Tanzania kutoa kauli zinazoibua hisia tofauti.

Mnamo mwaka 2017 Rais wa Tanzania John Magufuli alisema kuwa chini ya uongozi wake wasichana wa shule ambao hujifungua watoto hawataruhusiwa tena kurudi shuleni,
Rais magufuli alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara kwenye mji wa Chalinze, takriban umbali wa kilomita 100 magharibi mwa mji mkuu Dar es Salaam.
Magufuli anasema kuwa mwanamume ambaye atapatikana na hatia ya kumpachika mimba mtoto wa shule, atafungwa jela miaka 30 na kutumia nguvu alizotumia kumpachika mimba msichana huyo, kufanya kilimo akiwa gerezani.
"Mashirika haya yasiyo ya serikali yanastahili kuenda kufungua shule kwa wazazi, lakini hayastahili kuilazimisha serikali kuwarejesha shuleni.
"Ninatoa elimu ya bure kwa wanafunzi ambao wameamua kusoma, na sasa nataka niwaelimishe wazazi," Rais Magufuli alisema.
Kauli za Bwana Magufuli ziliibua hisia kali miongoni mwa watetezi wa haki za wanawake waliopinga kauli hiyo.
Nchini Tanzania kuna takriban wasichana 8,000 ambao huacha shule kila mwaka kutokana na kuwa wajawazito, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Human Rights Watch.
Magufuli aliwahi kuwahimiza wanawake wa Tanzania kutofunga vizazi vyao ili kuweza kuzaa watoto wengi kama njia mojawapo ya kupiga jeki uchumi wa taifa hilo kwa ili kuwa taifa lenye uchumi mkubwa Afrika mashariki , hatua ambayo wakosoaji wanasema itasababisha ukosefu wa usawa na kuleta umasikini kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
''Wakati unapokuwa na idadi kubwa ya watu unajenga uchumi . Ndio kwa sababu uchumi wa China ni mkubwa'' , alisema Mwezi Julai mwaka akitoa mfano wa mataifa kama vile India na Nigeria kama mataifa yalioimarika kiuchumi kutokana na idadi kubwa ya raia.
''Najua kwamba wale wanaopendelea kufunga vizazi watalalamika. Lakini wekeni huru vizazi vyenu, wawacheni wafunge vyao'', aliambia umati mkubwa wa watu nyumbani kwake huko Chato, alisema rais huyo wa Tanzania.

Post a Comment

0 Comments