tangazo

Rekodi za mauaji ya Jamal Khashoggi zachapishwa

Waandamanaji wakibeba bango la picha ya Khashoggi nje ya ubalozi wa saudia mjini Istanbul

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionGazeti hilo linasema kwamba Jamal Khashoggi (kwenye picha aliambia wauaji wake kutomfunga mdomo
Gazeti moja la Uturuki limechapisha maelezo mapya ya rekodi ambazo zinadaiwa kunaswa muda wa mwisho wa mwandishi wa Saudia Jamal Khashoggi.
Mkosoaji huyo maarufu wa serikali ya Saudia aliuawa katika ubalozi wa Saudia nchini Uturuki mwezi Oktoba.
Gazeti linalounga mkono serikali linasema kwamba hati hiyo inatoka katika rekodi zilizochukuliwa ndani na baadaye kuchukuliwa na idara ya ujasusi ya Uturuki.
Inashirikisha habari kama vile maneno ya mwisho ya mwandishi huyo.
Khashoggi aliandika hoja katika gazeti la Washington Post na alikuwa akiishi Marekani kabla ya kutoweka kwake.
Mara ya mwisho alionekana akiingia ubalozi wa Saudia mjini Instanbul tarehe 2 mwezi Oktoba 2018 ili kuchukua stakhabadhi baada ya kutaka kumuoa mpenzi wake wa Uturuki.
Kifo chake cha kushangaza kilizua hofu dhidi ya Saudia ambayo baadaye ilitoa habari za kutatanisha kuhusu kutoweka kwake.
Mamlaka ya Saudia kufikia sasa imeshtumu njama mbaya ya muaji yake na kuwashtaki watu 11.

Je gazeti hilo linasema nini?

Gazeti la Sabah limeendelea kugonga vichwa vya habari kimataifa kwa kuweka maelezo - ikiwemo mengine ambayo yamepinga mauaji ya kushangaza ya mwandishi hiyo.
Gazeti hilo lilichapisha ripoti mpya mbili zaidi wiki hii kuhusu kifo cha Khashoggi kilichodaiwa kutekelezwa na kundi moja kwa jina Hit Squad.
Ripoti zake za hivi karibuni zinaelezea kuhusu habari kutoka kwa rekodi hizo.
Zinashirikisha maelezo kama vile utaalamu wa kijasusi, kundi moja lililotumwa kutoka Saudia lililomtaja mwandishi huyo kuwa mnyama aliyehitaji kuchinjwa kabla ya kuwasili kwake.
Gazeti hilo linasema kwamba baada ya Khashoggi kuingia katika ubalozi huo alianza kuwa na hofu na aliambiwa kwamba alihitaji kurudi Riadh kutokana na agizo la polisi wa kimataifa.
Mwandishi huyo alidaiwa kukataa kufuata ombi hilo lililoshirikisha kutuma ujumbe kwa mwanawe wa kiume na ndiposa alipowekewa dawa za kulevya kulingana na gazeti hilo.
Aliripotiwa akiwaambia wauaji wake, katika maneno yake ya mwisho 'wasimzuia kufunga mdomo' kwa kuwa anakabiliwa na pumu lakini baadaye akapoteza fahamu.
Khashoggi alikoseshwa hewa baada ya kichwa chake kutiwa katika mfuko , gazeti hilo liliripoti huku sauti za mgogoro zikinakiliwa katika rekodi hiyo .
Gazeti hilo limedai kanda hiyo ilirekodi kukatwa katwa kwake mbele ya majasusi hao.
Ripoti kuhusu kuwepo kwa sauti za rekodi ya mauaji ya Khashoggi zimekuwepo tangu mwaka uliopita.
Maafisa wa Uturuki wamethibitisha wazi kuhusu kuwepo kwake na wanasema wamezisambazia mataifa , lakini haijulikani ni vipi gazet hilo lilifanikiwa kuzipata.
Mwaka mmoja baada ya kifo chake , mwiili wa Khashoggi haujapatikana licha ya shinikizo za kimataifa.
Mapema mwaka huu, watalaam wa Umoja wa mataifa kuhusu mauaji ya kiholela waliitisha uchunguzi huru usiopendelea kuhusu kifo chake.
Mjumbe maalum Agnes Callamard alitaja kifo cha mwandishi huyo kuwa cha makusudi , na kilichopangwa na kudai kwamba taifa la Saudia ndio lililohusika na kwamba linahitaji kuchunguzwa.
Serikali ya Saudia ilipinga ripoti yake na imeendelea kukana kwamba waliohusika walikuwa wakitekeleza maagizo ya maafisa wakuu serikalini
Agnes Callamard


Post a Comment

0 Comments