tangazo

Taifa Stars kuvaana na Burundi leo, rekodi zao zipo hiviTimu ya taifa ya Tanzania leo inaumana na Burundi katika mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kucheza katika kombe la dunia 2022 nchini Qatar.

Takwimu za michezo mitano iliyopita iliyowakutanisha Tanzania na Burundi, Stars imeshinda mechi mbili, sare moja na kupoteza mechi mbili.

Mara ya mwisho timu hizi zilikutana kwenye mchezo wa kirafiki Machi 28, 2017, Uwanja wa Taifa Dar es salaam, ambapo stars walishinda 2-1, magoli yakifungwa na Simon Msuva dakika ya 22, Mbaraka Abeid dakika ya 78 wakati goli pekee la Burundi lilifungwa na Laudit Mavugo dakika ya 54.

Post a Comment

0 Comments