tangazo

Teknolojia ya habari na mawasiliano ina nafasi kubwa - Dk. Shein


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kwamba teknolojia ya habari na mawasiliano ina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko ya maendeleo katika Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola.

Rais Dk. Shein aliyasema hayo katika ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Chama Cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya  Madinatul Bahr, iliyopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Rais Dk. Shein alisema kwamba iwapo teknolojia ya habari na mawasiliano itatumika ipasavyo hasa katika kuimarisha kanzi data mbali mbali hatua hiyo itarahisisha suala zima la kufanya maamuzi kwa wakati na kuweza kufikia malengo yaliokusudiwa.

Aliongeza kuwa uendeshaji wa Bunge kwa kutumia njia za kisasa kunawaweka karibu zaidi Wabunge na wananchi, jambo  ambalo linatoa fursa pana zaidi kwa wananchi ya ya kutoa maoni yao na hoja mbali mbali za maendeleo zinazogusa maisha yao ya kila siku.

Alieleza kuwa Bunge Mtandao ni nyenzo nzima ya kupunguza harama za mambo mbali mbali kama vile usafiri sambamba na kuokoa muda.

Post a Comment

0 Comments