Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 13.09.2019:

 Maddison, Ruiz, Kante, Aurier, Terry, Lindelof, Vardy, Bolasie


Ngolo KanteHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane atanataka kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea N'Golo Kante, 28. (The Athletic, subscription required)
Manchester United wanamchunguza kiungo wa kati wa Leicester City James Maddison kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 msimu ujao. (Manchester Evening News)
Mshambuliaji wa zamani wa England Wayne Rooney anaamini Pep Guardiola angeshinda vikombe vyote iwapo angepewa ukufunzi wa timu ya Uingereza. (Manchester Evening News)

Pep Guardiola

Liverpool, Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich zinamnyatia kiungo wa kati wa Napoli Fabian Ruiz, 23. (Calciomercato, via Daily Mail)
Nahodha wa zamani wa klabu ya Chelsea John Terry amepigiwa upatu na mkufunzi wa zamani Roberto Di Matteo kuwa mkufunzi wa klabu hiyo katika siku za usoni. (Athletic, via Birmingham Mail)
Mshambuliaji wa Chelsea Willian anaamini timu yake ina uwezo wa kushinda taji msimu huu licha ya mkufunzi mpya Frank Lampard kushika hatamu katika hali ngumu. (Standard)

Willian

Manchester United imeandaa kuongeza maradufu mshahara wa Victor Lindelof, 25, na kumpatia kandarasi ya mshahara wa £150,000 kwa wiki. (Sun)
Mkufunzi wa England Gareth Southgate anasema kwamba mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy huenda akarudi katika kikosi cha taifa licha ya kutangaza kustaafu kutoka soka ya kimataifa mwaka uliopita . (Times, subscription required)
Beki wa zamani wa Arsenal Per Mertesacker ametoa wito kwa kiungo wa kati Asrenal Mesut Ozil, 30, kuimarika na kutoa mchango wake kwa klabu hiyo , akisema kwamba ana kipaji ambacho hakina mchezaji mwengine wa Arsenal. (Talksport)

Mesut OzilHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Beki wa kulia wa Tottenham Serge Aurier, 26, amekiri kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu huu.. (Football.London)
Winga wa Everton Yannick Bolasie, 30, ambaye kwa sasa yuko katika klabu ya Sporting Lisbon, anatumai kwamba kandarasi yake itafanywa kuwa ya kudumu msimu ujao. (Record, via Sport Witness)

TETESI ZA SOKA ALHAMISI


Tottenham huenda ikabadilishana kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen,

Tottenham huenda ikabadilishana kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27, na mshambuliaji wa Juventus' raia wa Argentina Paulo Dybala, 25, wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Tuttosport, via Express)
Kiungo wa kati wa Manchester Paul Pogba, 26, amekubali malipo ya mahshara wa £429,000 kwa wiki na Paris St-Germain kabla ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho lakini uhamisho huo uligonga mwamba baada ya Neymar kushindwa kuhamia Barcelona. (Calciomercato, via Sun)
Real Madrid na Chelsea wameafikiana makubaliano ya uhamisho wa kiungo N'Golo Kante, 28, ambapo klabu hiyo itaambia klabu hiyo ya Uhispania iwapo watapokea maombi yoyote ya mchezaji huyo wa Ufaransa. (Defensa Central, via Express)

N'golo Kante

Mchezaji anayelengwa na Tottenham Bruno Fernandes, 25, huenda akapatikana huku Sporting Lisbon ikiwa tayari kumuuza kiungo huyo wa kati kwa dau la £62m. (A Bola, via Sport Witness)
Kungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 28, angependelea kujiunga na mchezaji mwenzake wa zamani Vincent Kompany katika klabu ya Anderlecht wakati atakapoondoka Manchester City. (Sky Sports)
Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger amefichua kwamba alijaribu kumsaini Jadon Sancho, 19, wakati winga huyo alipokuwa Manchester City kabla ya kuelekea kujiunga na klabu ya Borussia Dortmund. (Express)

Arsene Wenger

Mchezaji wa Chelsea aliyepo kwa mkopo Victor Moses, 28, huenda asitie saini mkataba wa kudumu katika klabu ya Fenerbahce, licha ya klabu hiyo ya Uturuki kuwa na fursa ya kumnunua winga huyo wa Nigeria . (Star)
Manchester United huenda ikamruhusu mkufunzi wake Ole Gunnar Solskjaer kumnunua kiungo wa kati katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku bodi ya klabu hiyo ikiweka fedha tayari kupiga jeki kikosi hicho katikati ya msimu.. (Manchester Evening News)
Winga wa zamani wa England Trevor Sinclair anasema kwamba kiwango cha mchezo cha mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling ni kizuri sawa na kile cha Lionel Messi na Cristiano Ronaldo's. (Talksport)

Raheem SterlingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Sterling, 24, anatarajiwa kuorodheshwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa vizuri kibiashara huku kampuni ya Pepsi ikimtumia katika tangazo ambalo yeye ameshirikishwa pamoja na Paul Pogba na Lionel Messi . (Telegraph)
Mshambuliaji wa Uhispania Inaki Williams, 25, amefichua kwamba aliwasiliana na Man United kabla ya kutia saini mkatava mpya na klabu ya Athletic Bilbao. (Cadena Ser, via Independent)
Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson ameonya mashabiki wa klabu hiyo kwamba huenda kukawa na 'mateso na maumivu ya moyo' katika uwanja huo wa Selhurst Park msimu huu. (Standard)

TETESI YA JUMATANO


Leoroy Sane

Manchester City inajaribu kumshawishi mshambuliaji wake Leroy Sane, 23, kutia saini kandarasi mpya kabla ya Bayern kupewa fursa nyengine ya kuwasilisha ombi la kumsaini raia huyo wa Ujerumani . (Standard)
Chelsea itajaribu kumsaini beki anayedaiwa kuwa na thamani ya £35m kutoka klabu ya Nice Youcef Atal, raia wa Algeria mwenye umri wa miaka 23 mwezi Januari iwapo watafanikiwa kuondolewa marufuku yao ya uhamisho kuanzia mwanzo wa 2020. (Sun)
Manchester United inamnyatia kiungo wa kati wa Benfica na Portugal Florentino Luis, 21, lakini anaweza kukabiliwa na ushindani wa kumsaini kutoka kwa klabu ya Manchester City (A Bola via Sport Witness - in Portuguese)

Florentino Luis,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Kiungo wa Real Betis na Ufaransa Nabil Fekir, 26, amekana madai kwamba uhamisho wake wa dau la £53m kuelekea Liverpool 2018 uligonga mwamba kutokana na kufeli kwa vipimo vya matibabu.. (L'Equipe, via Talk Sport)
Manchester City ilifeli katika ombi lake la kumsaini beki wa inter Milan raia wa Slovakia Milan Skriniar, 24, lakini inaweza kujaribu tena mwezi Januari. (Tuttosport, via Sport Witness)
Kiungo wa kati wa Armenia ambaye aliwahi kuzichezea Manchester United na Arsenal Henrikh Mkhitaryan, 30, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Roma amesema kwamba kipindi chake cha mchezo katika ligi ya Premia kilimfanya kukosa mapenzi na kandanda. (Manchester Evening News)

Henrikh Mkhitaryan

Chelsea itajaribu kumsaini beki wa kushoto wa Valencia na Uhispania Jose Gaya, 24, wakati marufuku ya dirisha la uhamisho itakapokamilika msimu ujao. (Soccer Link, via Talk Sport)
Beki wa zamani wa Arsenal na Ujerumani Per Mertesacker, 34, anaamini wachezaji wa klabu hiyo walishindwa kutoa ushahidi wa kuwepo kwa imani ya Wenger katika siku za mwisho za mkufunzi huyo wa zamani wa Arsena(Standard)
Kiungo wa kati wa Brazil Lucas Piazon, 25, anasema yuko tayari kuondoka Chelsea kabisa kwa kuwa amechoshwa na hatua ya kuuzwa kwa mkopo kila mwaka. (A Bola, via Goal)

Lucas Piazon

Arsene Wenger anasema kwamba majuto yake makubwa akiifunza Arsenal ni kushindwa kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi. (beIN Sports)
Mkufunzi wa taasisi ya soka ya Crystal Palace Shaun Derry amefichua jinsi siku nne za kuichezea klabu ya Cambridge United zilivyomfanya beki wa England Aaron wan Bissaka kushawishika kuanza safari yake kuelekea Man United. . (Standard)

TETESI ZA SOKA JUMANNE


Douglas CostaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Juventus imekataa kumuuza winga Douglas Costa 28 licha ya Man United kuwa na hamu ya kumsajili baada ya mkufunzi Maurizio Sarri kuzuia uhamisho wa nchezaji huyo wa Brazil. (Mail)
Real Madrid itawasilisha ombi la kumsaini kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen msimu ujao iwapo Paul Pogba ataongeza kandarasi yake na Man United .
Eriksen mwenye umri wa miaka 27 atapatikana kwa uhamisho wa bila malipo kwa kuwa kandarasi yake inakamilika 2020. (Sky Sports)

Paul Pogba

Beki wa Real Madrid Sergio Ramos amemshauri Pogba, 26, kutoka Man United na kuhamia katika klabu hiyo ya Uhispania. (Express)
Chelsea imeanzisha mazungumzo na beki wa Itali Emerson, 25, kuhusu kandarasi mpya mpya. Winga wa England Callum Hudson Odoi 18 anakaribia kukamilisha mkataba mpya wa malipo ya £180, 000 kwa wiki katika mkataba wa miaka mitano.. (Express)

Hudson OdoiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Tottenham iliwatuma wawakilishi ili kumtazama mshambuliaji wa Fenerbahce Vedat Muriqi, 25, akiichezea Kosovo wikendi iliopita.
Maskauti kutoka Lazio, Fiorentina na Napoli pia walikuwepo huku Muriqi akifunga katika ushindi wa Kosovo wa 2-1 dhidi ya Czech Republic. (Sabah, via Four Four Two)
Mlinda lango wa Manchester United David de Gea, 28, anakaribia kutia kandarasi mpya ambayo itampatia mshahara wa £290,000 kwa wiki ikiwa ni mshahaha anaolipwa Pogba. (Guardian)
Mchezaji wa timu ya Itali ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Paolo Nicolato amemwambia mshambuliaji wa Everton Moise Kean kujifunza kutokana na makosa baada ya kuwasili kuchelewa katika mkutano wa timu kabla ya mechi dhidi ya Ubelgiji.

Mise Kean wa EvertonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Kean 19 aliwachwa nje kutoka katika kikosi cha Itali katika mechi za kimataifa za hivi karibuni (Gazzetta Dello Sport, via Sport Witness)
Tottenham ilitaka kumsaini kiungo wa kati wa Roma Nicolo Zaniolo, 20, kulingana na ajenti wa mchezaji huyo kabla ya kumsaini Giovani lo Celso kwa mkopo badala yake. (Mail)
Wolves ilifeli kumsaini kiungo wa kati Leeds Kalvin Phillips msimu huu ,ilibainika baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kutia kandarasi mkataba mpya katika klabu hiyo.. (Football Insider)

Giovani lo Celso

Chelsea imeambia maajenti wake wakuu kwamba inaamini kwamba marufuku ya uhaimsho waliowekewa inayowazuia kununua wachezaji msimu huu itapunguzwa , ikimaanisha kwamba wanaweza kununua wachezaji katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Newcastle Jonjo Shelvey, 27, ametaja baadhi ya ukosoaji dhidi Steve Bruce na klabu hiyo kama upuzi na aibu. (Chronicle)

Steve Bruce wa Newcastle

Klabu ya ligi ya Bundelsiga Paderborn huenda inataka kufanya jaribio la pili la kumsaini kiungo wa kati wa Crystal Palace Jairo Riedewald, 23, mnamo mwezi Januari baada ya kukosa uhamisho wa mkopo msimu huu . (Football.London)
Beki Jesus Vallejo, 22, aliyejiunga na Wolves kwa mkopo katika dirisha la uhamisho la msimu huu anaweza kuuzwa na klabu ya Real Madrid msimu ujao. (Birmingham Mail)
Tamasha kwa jina A Cirque du Soleil kuhusu mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi liitaanza katika mji wa Catalan mwezi Oktoba. (Standard)
TETESI ZA SOKA JUMATATU

Barcelona wanajiandaa kusaini mkataba na mshambuliaji wa mbele Lionel Messi, 32Haki miliki ya pichaAFP
Image captionBarcelona wanajiandaa kusaini mkataba na mshambuliaji wa mbele Lionel Messi, 32

Barcelona wanaandaa mkataba mpya wa mshambuliaji Lionel Messi, 32, ambao utambakisha nyota huyo Camp Nou kwa miaka iliyosalia ya maisha yake ya soka. (Mundo Deportivo via Mirror)
Chelsea inaweza kulazimika kumpa mkataba wa muda mrefu beki wake wa kushoto Mbrazil Emerson Palmieri, mwenye umri wa miaka 25, ambaye kocha Maurizo Sarri anamyemelea kumpeleka Juventus. (Express)
Manchester United na Manchester City wapo mbioni kupambana kumsajili kiungo wa wa Benfica Florentino Luis mwenye umri wa miaka 20. (Star)

Paul PogbaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPaul Pogba

Kiungo nyota wa Ufaransa Paul Pogba, 27, aliamua kusalia Manchester United badala ya kuhamia Real Madrid kutokana na mkataba wa pauni pauni 150 wa udhamini wa michezo . (The Sun)
Beki wa timu ya taifa ya Uholanzi Virgil van Dijk, 28, ameshangazwa na maneno kuwa atapewa ofa ya mpya ya mkataba wa malipo ya pauni na 200,000 kwa wiki na klabu yake ya Liverpool. (Liverpool Echo)
Kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 24, anakaribia kusaini mkataba mpya licha ya Manchester United kumtaka Mserbia huyo pamoja na vilabu vya Paris St-Germain na Juventus. (Daily Mail)

Mchezaji wa safu ya ulinzi ya Uholanzi Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 28Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMchezaji wa safu ya ulinzi ya Uholanzi Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 28

Meneja wa zamani wa Leicester Mfaransa Claude Puel ndiye mtu anayetazamiwa kuchukua nafasi ya meneja katika klabu ya Ureno ya Sporting Lisbon.(L'Equipe)
Marcos Rojo, 29, atalazimisha kuhamia Aston Villa kutoka Manchester United mwezi Januari , baada ya mlinzi huyo wa Argentina kushindwa kuondoka Old Trafford katika dirisha la usajili lililoisha hivi karibuni. (Birmingham Live)
Kelechi Nwakali, 21, ambaye alihamia katika klabu ya daraja la pili ya Uhispania, Huesca kutoka Arsenal msimu huu , anataka kurudi katika uwanja wa Emirates siku zijazo . (Score Nigeria via Football.London)
Beki wa England Danny Rose, 29, anataka kuendela kupigania nafasi yake katika timu ya Tottenham Hotspur licha ya kwamba klabu nyingine zimeonyesha kumtaka na kuwasili kwa Ryan Sessegnon, mweny umri wa miaka 19, kutoka Fulham. (Mirror)

Marcos Rojo, mwenye umri wa miaka 29, atalazimika kuhamia Aston Villa kutoka Manchester United mwezi JanuariHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMarcos Rojo, mwenye umri wa miaka 29, atalazimika kuhamia Aston Villa kutoka Manchester United mwezi Januari

Real Madrid watagrejelea tena haja yao ya kumsaka kiungo wa kati wa Ajax - Donny van de Beek,mwenye umri wa miaka 22, katika kipindi cha msimu kuhama kwa wachezaji cha majira ya kiangazi cha mwaka 2020 . (Daily Mail)
Leeds wanakaribia kabisa kuongeza zaidi mkataba wa miaka mitano na kiungo wa kati wa Kalvin Phillps mwenye umri wa miaka 23 ,baada ya Aston Villa na Burnle kuonyesha nia za kumnunua mchezaji huyo katika kipindi cha mechi za kipindi cha kabla ya kuaza kwa msimu wa michezo . (Telegraph)
Mchezaji wa safu ya nyuma wa Italy ukipenda full-back -Matteo Darmian, mwenye umri wa miaka 29, anasema hajutii kitendo chake cha kuhamia Manchester United,paada ya kujiunga na Parma kuhfuatia misimu minne akiwa katika Old Trafford. (Football Italia)
Mlinda lango wa Stalwart Germany na Bayern Munich Manuel Neuer, mwenye umri wa miaka 33, hana mipango ya kustaafu . (Mirror)
Waziri mkuu wa Albania Edvin Rama amefichua kuwa mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron aliomba msamaha wa dhati baada ya kupigwa kwa wimbo wa taifa ambao sio wa Albania kwa ajili ya timu ya nchi yake katika mchezo wa timu zilizofuzu kwa ajili ya kombe la Euro 2020 wakati wapocheza na timu ya Ufaransa mjini Paris. (Goal.com)

Post a Comment

0 Comments