TFF na Azam Media wasaini mkataba wa miaka minne wenye thamani ya Tsh. Bilioni 4.5



Shirikisho la soka nchini Tanzania limesaini mkataba wa miaka minne na kampuni ya Azam Media kwa ajili ya kuonesha moja kwa moja mechi za Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Mkataba wa awali wa Azam Sports umefikia tamati msimu uliopita na sasa pande hizo zimesaini mkataba mpya wa miaka minne wenye thamani ya shilingi bilioni 4.5.

Pia mkataba wa kuonesha mechi za Taifa Stars umegharimu shilingi milioni 400 ambazo ni sawa shilingi milioni 100 kwa mwaka, na kwenye kila mechi Taifa Stars itapata shilingi milioni 35 kutoka Azam Media.

Akitoa ufafanuzi wa mkataba huo Mkuruguenzi wa Michezo wa Azam Media Patrick Kahemele amesema mechi za Taifa Stars zilizodhamini na Azam ni zile za kirafiki zitakazokuwa kwenye kalenda ya FIFA.



Post a Comment

0 Comments