tangazo

Ufaransa: Kampuni yaingia hatiani baada ya kufariki akifanya mapenzi


Stock photo of man and womanHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kampuni moja nchini Ufaransa imejikuta na hatia kwa kifo cha mfanyakazi wake aliyekuwa na tatizo la moyo kukutwa na mauti wakati akifanya mapenzi alipokuwa katika safari ya kikazi.
Mahakama ya mjini Paris imetoa hukumu kuwa kifo cha mfanyakazi huyo kilitokea akiwa kazini hivyo hiyo ni ajali kazini na lazima famila ilipwe na kampuni.
Licha ya kwamba kampuni kudai kuwa mfanyakazi huyo mauti ilimkuta wakati akiwa afanyi shughuli za kampuni kwa kumkaribisha mwanamke asiyemjua kulala naye hotelini
Lakini sheria ya wafanyakazi nchini Ufaransa, mfanyakazi anapaswa kulipwa pale anapopata ajali akiwa safari ya kikazi, jaji alieleza.
Mwanaume huyo aliyepewa jina la Xavier X, alikuwa muhandisi katika kampuni ya reli iliyopo Paris.
Wapenzi kitandaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mfanyakazi huyo alifariki mwaka 2013, baada ya kukutwa akiwa anafanya mapenzi na mtu asiyemfahamu.
Kampuni hiyo ilipinga maamuzi hayo kwa kuwalalamikia watoa huduma ya bima ya afya kudai kifo hicho ni ajali kazini.
Nao watetezi wa kesi hiyo walidai kuwa mtu kufanya mapenzi ni jambo la kawaida sawa na mtu kwenda kuoga au kula chakula.
Hukumu imetoka na kudai kuwa mtu yeyote aliyeenda safari ya kikazi anapaswa kulindwa na kampuni wakati wote.

Post a Comment

0 Comments