tangazo

Uingereza: Soko la mtandaoni laathiri biashara ya maduka

maduka

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMaduka yapatayo 3000 yaliyoko maeneo ya mijini nchini Uingereza yamefungwa mwaka huu
Ni nadra sana mwezi kupita bila taarifa juu ya maduka kufungwa kutangazwa au kuwepo kwa madai kuwa maduka yanapata hasara.
Maduka yapatayo 3000 yaliyoko maeneo ya mijini nchini Uingereza yamefungwa mwaka huu.
Kukua kwa kasi kwa biashara ya mtandaoni kutokana na matangazo na urahisi wa kununua bidhaa katika mtandao ndio sababu inayowafanya wateja kupunguza kwenda dukani kwa ajili ya manunuzi.
Kumiliki duka bila kutumia mitandao ni hasara ndio maana rekodi ya maduka yaliofungwa au yasiyo na vitu yameo.
Women carrying shopping bagsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Ni zaidi ya asilimia kumi ya maduka kufungwa imeongezeka tangu Januari 2015.

Watu wamebadili namna ya kufanya manunuzi

Kwa namna nyingi ,bidhaa zinaweza kuuzwa kiurahisi. Ingawa unapaswa kuuza kwa gharama ya zaidi ya bei uliyonunulia au kugharamikia.
Miaka ya hivi karibuni biashara imekuwa ngumu kwa wauzaji wa maduka wanaosubiria wateja kufika dukani.
Debenhams storefrontHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Makampuni au maduka hayo yanapaswa kukabiliana na ongezeko la gharama, kuanzia kwenye kodi ya jengo na mzunguko wa biashara.
Wakati huohuo wafanyabiashara wakijaribu kuendana na mabadiliko ya tabia za wateja.
Wateja siku hizi wanatumia kila fedha yao katika mtandao - na kama biashara zinaonekana kuwa na mauzo hafifu kwa asilimia ishirini licha ya kwamba gharama za uendeshaji biashara zimeongezeka , na kufanya upatikanaji wa faida kuwa mdogo.
Mfumo mpya wa manunuzi na uuzwaji wa bidhaa katika biashara siku hizi unawapa wakati mgumu wafanyabiashara wengi ambao wanashindwa kuendana na mabadiliko hayo.
Wamiliki wengi wa maduka wanabaki kuwa na deni kubwa kutokana na kushindwa kuendesha biashara zao vizuri.
Aina ya maisha ambayo watu wamechagua inawagharimu haswa kwa bidhaa ambazo haziwezi kukaa kwa muda mrefu.
Kuwa na bidhaa zenye ubora mzuri sio kigezo tena kwa watu kuja kutembelea duka lako.
Debenhams storefrontHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Hali ya hewa pia ni sababu nyingine inayosababisha watu kuacha kwenda dukani.
Pamoja na kwamba watu bado wanafanya manunuzi lakini kukua kwa mitandao , maduka yanapaswa kuwafuata watu katika makwao na sio wateja kufuata maduka.
Mabadiliko haya yamepelekea watu kupoteza ajira zao kwa wingi.
Toys R UsHaki miliki ya pichaPA
Mwaka huu, watu zaidi ya 1,000 wamepoteza ajira zao haswa katika maduka makubwa ya nguo.
Inatajwa kuwa ndani ya miaka miwili, watu wengi zaidi watapoteza ajira zao na idadi inaweza kufika hata 900,000 katika karne ijayo.
Maduka ambayo yanaendelea kufunguliwa ni yale ya kupeleka chakula au maeneo ya kufanya mazoezi.
Wachambuzi wa mambo wanadai kuwa watu wanaacha utamaduni wa zamani wa manunuzi kwa sababu ya maeneo ambayo maduka mengi yamefunguliwa.
Hivyo watakaoweza kushinda katika biashara hii ni kufuata kile ambacho wateja wanakitaka huduma waipate na waweze kununua.

Post a Comment

0 Comments