Visima vya mafuta vya Saudia vyachomeka kutokana na shambulio.


Kisima cha mafuta nchini Saudia chalipuliwa

Shambulio la ndege zisizokuwa na rubani limechoma hifadhi mbili za mafuta zinazomilikiwa na kampuni ya serikali ya taifa la Saudia Aramco , kulingana na vyombo vya habari.
Kanda za video zilionyesha moto mkubwa katika eneo la Abqaiq ikiwa ndio hifadhi kubwa ya mafuta ya Saudia huku shambulio la pili likichoma moto hifadhi ya mafuta ya Khurais.
Moto huo kwa sasa umedhibitiwa katika hifadhi zote mbili , kulingana na vyombo vya habari.
Msemaji wa kundi la Houthi linaloungwa mkono na Iran nchini Yemen amesema kwamba walirusha ndege kumi zisizo na rubani katika shambulio hilo.
Msemaji waasi hao Yahya Sare aliambia runinga ya al-Masirah ambayo inamilikiwa na waasi hao wa Houthi kwamba mashambulio zaidi yanafaa kutarajiwa katika siku za usoni.
Alisema kwamba shambulio hilo la siku ya Jumamosi ndio kubwa zaidi kuwahi kutekelezwa na wapiganaji hao ndani ya Saudia na kwamba lilitekelezwa kupitia usaidizi wa baadhi ya raia wa ufalme huo.
Maafisa wa Saudia hawajatoa tamko lao kuhusu ni nani wanayefikiria alihusika na shambulio hilo.

Ramani

Abqaiq iko takriban kilomita 60 kusini magharibi mwa Dhahran nchini Saudia huku Khurais ikiwa kilomita 200 kusini magharibi na ina kisima cha mafuta ambacho ni cha pili kwa ukubwa.
Vikosi vya Saudia viliharibu jaribio la wapiganaji wa Al Qaeda kushambulia Abqaiq kwa kutumia wapiganaji wa kujitoa muhanga 2006

Hatari ya kundi la Houthi

Jonathan Marcus, mwandishi wa maswala ya ulinzi wa BBC
Shambulio hili la hivi karibuni linaonyesha hatari inayoletwa na kundi la Houthi katika visima vya mafuta vya Saudia.
Uwezo wa Houthi wa kutekeleza mashambulio ya ndege zisizo na rubani huenda ukazua upya mjadala wa ni wapi wanapata uwezo kama huo.
Je wapiganaji hao wamezifanya ndege zisizo na rubani za raia kuwa na uwezo wa kubeba makombora ama wamepata usaidizi mkubwa kutoka kwa Iran?.
Utawala wa rais Trump utailaumu Iran kwa tukio hilo lakini wataalam wanatofautiana kuhusu kiwango cha uwezo ambao Iran unafadhili kampeni hiyo ya ndege zisizo na rubani.
Wanahewa wa Saudia wamekuwa wakishambulia baadhi ya maeneo nchini Yemen kwa miaka kadhaa sasa. Sasa Houthi wana uwezo wa kulipiza kisasi.
Inaonyesha kwamba miaka ya ndege zisizo na rubani zinazobeba silaha kumilikiwa na mataifa machache yenye uwezo umekwisha.
Teknolojia ya ndege zisizo na rubani inapatikana kila mahali kutoka China hadi Marekani , Israel hadi Iran na kutoka kwa Houthi hadi Hezbollah.

Kampuni ya mafuta ya Aramco

Aramco ndio kampuni kubwa ya mafuta duniani na visima hivyo vya mafuta ni muhimu .
Visima vya mafuta vya Khurais vinatoa asilimia 1 ya mafuta duniani na kisima cha mafuta cha Abqaiq ndicho kikubwa zaidi kikiwa na uwezo wa kutoa asilimia 7 ya mafuta yote duniani.
Tatizo lolote dogo linaweza kuathiri kampuni hiyo kutokana na ukubwa wake.
Lakini iwapo shambulio hilo litakuwa na athari katika bei ya mafuta kufikia siku ya Jumatatu itatagemea na kiwango cha uharibifu uliofanyika.
Masoko sasa yana wikendi hii kuchanganua hali ilivyo kutoka kwa Aramco na kuona athari yake ya muda mrefu.

Je wapiganaji wa Houthi ni akina nani?

Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya Yemen na muungano wa majeshi yanayoongozwa na Saudia.
Yemen imekuwa katika vita tangu 2015 , wakati rais Abdrabbuh Mansour Hadi alipolazimishwa kutoroka mji mkuu wa Sanaa na wapiganaji wa Houthi.
Saudia inamuunga mkono rais Hadi na imeongoza kampeni inayoshirikisha vikisi vya mataifa ya mashariki ya kati dhidi ya waasi hao.
Muungano huo hurusha makombora ya angani kila siku huku Houthi nao wakirusha makombora nchini Saudia.
Bwana Serea msemaji wa Houthi aliambia chombo cha habari cha Al- Masirah kwamba Operehseni dhidi ya Saudia itapanuka na kuwa chungu zaidi ya ilivyokuwa iwapo itaendeleza mshambulizi Yemen mbali na kuweka vizuizi.

Mahsmabulizi ya angani ya Saudia hulenga maficho ya Houthi Yemen.Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMahsmabulizi ya angani ya Saudia hulenga maficho ya Houthi Yemen.

Post a Comment

0 Comments