tangazo

ACT Wazarendo yajipanga kushiriki uchaguzi mkuu 2020

Chama cha ACT Wazalendo kimejipanga kushiriki na kushinda kwenye chaguzi wa Urais, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani ambao utafanyika mwaka huu.

Katika kipindi hiki ambapo wanachama wanasubiri ratiba ya uchukuaji fomu na vikao vya uteuzi wa wagombea, tunapenda kuwakumbusha wanachama wa ACT Wazalendo kuwa kanuni na taratibu za ACT Wazalendo zinaruhusu wanachama kutangaza nia ya kugombea nafasi wanazozitaka kwenye uchaguzi.

"Kama inavyofahamika, 2020 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani. Kwa upande wa Zanzibar, watachagua pia Rais wa Zanzibar na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi" Ado Shaibu.


Ofisi ya Katibu Mkuu inawakumbusha kuwa;

1. Kila mwanachama ana uhuru wa kujitangaza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu nia yake ya kugombea nafasi yoyote anayotaka kugombea kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

2. Makatibu wa Kata na Majimbo wameagizwa kuandaa madaftari ya watia nia katika maeneo yao ambayo kila mtia nia atajiorodhesha na kuandikisha taarifa zake.

3. Katika kutangaza nia, watia nia wanakumbushwa kuzingatia misingi ya maadili, utu na kanuni za uchaguzi za Chama chetu.

4. Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma imeagizwa kuhakikisha kuwa inatoa msaada kwa watia nia kujitangaza hasa kwa kuwaunganisha na vyombo vya habari.

Post a Comment

0 Comments