Baraza la Usalama kupitisha azimio kuhusu janga la corona



Baaada ya muda wa zaidi ya mwezi mmoja wa utatanishi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa wiki ijayo kupitisha azimio la kwanza juu ya janga la maambukizi ya corona.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kupitisha azimio hilo licha ya mivutano kati ya Marekani, China na Urusi. Jukumu hilo litatekelezwa? Jee mwito wa ushirikiano umefunikizwa na sera za kizalendo au hiyo ni hatua  ya kuelekea kwenye kuubadalisha Umoja wa Mataifa ulioundwa mnamo mwaka 1945 kwa lengo muhsusi  la kuzuia na kutatua migogoro ya kimataifa?
Wanadiplomasia na wataalamu waliojibu maswali ya shirika la habari la AFP hawakuonyesha matumaini makubwa. Baraza la Usalama limekuwa kimya juu ya janga kubwa kabisa lisilokuwa na kifani tangu kumalizika vita vikuu vya pili. Baraza hilo limekutana mara moja tangu kulipuka janga la corona. Lilifanya mkutano wake tarehe 9 mwezi huu wa April kutokana na pendekezo la Ujerumani na Estonia.

Lengo la Azimio:

Azimio lililopendekezwa kwa pamoja na Tunisia na Ufaransa linatoa mwito wa kuimarisha juhudi za pamoja baina ya mataifa yote pia linatoa mwito wa kukomesha uhamasa na mapigano kwenye maeneo ya mizozo. Lengo la azimio hilo ni kuunga mkono juhudi za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa yanayopambana ili kuzuia maakumbizi ya virusi vya corona na athari zake za kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Mkurugenzi wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia migogoro ya kimataifa, Richard Gowan amesema baraza la uslama linajaribu kujitoa kimasomaso kwa azimio hilo ili kujionyesha kuwa limechukua hatua. Hata hivyo amesema hatua hiyo haitaleta manufaa thabiti. Jee azimio hilo litaziwajibisha nchi zote wanachama na kuleta manufaa kwenye sehemu za mizozo kama vile Syria, Yemen, Mashariki ya Kati, Afghanistan, Colombia na katika baadhi ya nchi za barani Afrika? Kukomesha miogoro duniani ni jambo linalostahili pongezi lakini changamoto iliyopo ni namna ya kufikia kwenye lengo hilo kwa kila nchi. Hayo amesema mwanadiplomasia mmoja ambae hakutaka kutajwa jina.

Post a Comment

0 Comments