CORONA TANZANIA: Visa vyafikia 306 “wagonjwa 84 wamepona”

Wizara ya Afya Zanzibar imetoa taarifa ya ongezeko la Wagonjwa wapya saba wa corona na kufikisha idadi ya wagonjwa 105 kutoka 98, wagonjwa wote wapya ni Raia wa Tanzania na wametokea Unguja, kwa ongezeko hili sasa idadi ya visa vya corona Tanzania nzima imefikia 306 kutoka 299.
Wizara ya Afya Zanzibar pia imesema wagonjwa 36 wa corona wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku wakishauriwa kubaki katika nyumba zao kwa siku 14 kabla ya kurudi kwenye shughuli zao, kwa ongezeko hili sasa idadi ya waliopona corona Tanzania nzima imefikia 84 kutoka 48.

LIVE MAGAZETI: MWILI WA DC MTWARA KUZIKWA NA WATU 10, FAMILIA YAZUIA MWILI WA MEYA KUZIKWA NA SERIKALI

Post a Comment

0 Comments