Kampeni za uchaguzi zaanza rasmi nchini Burundi

Kampeni za uchaguzi wa urais utakaofanyika Mei 20 zimeanza leo nchini Burundi ambapo mgombea urais kupitia chama tawala CNND-FDD, Evariste Ndayishimiyena na Agathon Rwasa wa chama cha upinzani, CNL wamezindua kampeni zao
Mkuu wa Tume ya Uchaguzi, Pierre Claver Kazihise, amewaonya vikali wale wote watakaokwenda kinyume na sheria, huku waziri wa afya akiwakumbusha wagombea na raia kuzingatia kanuni za kuepukana na ugonjwa wa COVID-19. 

SAUTI NA VIDIO KUHUSU MADA

dakika (0)
IDHAA YA KISWAHILI | 27.04.2020

J3 27.04 Burundi aktuell - MP3-Stereo

Ni katika tarafa ya Bugendana mkoani Gitega kati mwa nchi, ndiko Evariste Ndayishimiye mgombea wa chama cha CNDD-FDD alikoanzia kampeni akiwa pamoja na vigogo wa chama hicho, akihudhuria pia Rais Pierre Nkurunziza, mwenye cheo cha kiongozi wa milele wa chama hicho.
Wafuasi wa chama wameonekana wakivalia sare za chama hicho zilochapishwa: Tumpigiye kura Evariste Ndayishimiye. Mgombea huyo wa chama tawala tayari amepata uungaji mkono kutoka vyama vya FNL kinachoongozwa na Jaques Bigirimana, muungano wa COPA, na wafuasi wa UPRONA wanaoelemea kundi la Isidore Mbayahaga..

Post a Comment

0 Comments