Maambukizi ya virusi vya corona yapindukia watu milioni 3 duniani


Rekodi mpya visa vya maambuziki ya virusi vya corona hadi sasa inaonesha vimepindukia watu milioni tatu  duniani kote, ambapo karibu asilimia 80 vimerekodiwa Ulaya na Marekani.
Wakati hali ikiwa hivyo, Umoja wa Mataifa ukisema kunahitajika kitita cha kiasi cha dola bilioni 90 ili kunusuru jumla ya watu milioni 700 walioathirika zaidi wakiwemo wa katika maeneo masikini, ambayo kilele cha maambukizi hayo bado hakijafikia.
Kwa takwimu za shirika la habari la AFP  takribani maambukizi 3,003,344 yamebainika, ikiwemo vifo 209,388, na vingi vya hivyo vimetokea Ulaya ambako kuna jumla ya maambukizi 1,393,779 na vifo 126,233. Marekani kuna maambukizi 980,008 vikiwemo vifo 55,637.  Mkuu wa ofisi ya misaada ya kibinaadamu ya Umoja wa Mataifa Mark Lowcock amesema kiasi hicho cha dola bilioni 90 ambaco amependekeza kitolewe kwa masharti nafuu kinaweza kusaidia katika kuongeza kipato, chakula na afya kwa  jamii ya takribani watu 700 iliyo katika hatari zaidi.

Mashiriki ya kimataifa kuwa wafadhili wakuu

Amesema pamoja na wafadhili wengine  theluthi mbili za kiasi hicho cha bilioni 90 kitatolewa na taasisi za kifedha za kimataifa kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani IMF. Katika taarifa yake kwa njia ya video alisema kilele cha COVID-19 hakijafika katika katika maeneo masikini zaidi lakini alikiwa hali inaweza kuwa tofauti katika kipindi cha wiki miezi mitatu hadi sita toka sasa. Na katika hatua nyingine Rais Donald Trump wa Marekani ameilaumu China kwa kusema taifa hilo lingweza kudhibiti kusambaa kwa virusu vya corona kabla havijavuta mipaka ya taifa hilo. Kutokana na hali hiyo anasema serikali yake imeanzisha uchunguzi makini wa kile kilichotokea.

Wagonjwa 12 wa mwisho wa Wuhan watolewa hospitali


Post a Comment

0 Comments