Makabiliano kati ya Iran na Marekani yazua hofu ya kuzuka kwa vita Ghuba

Mwaka uliopita , rais Donald Trump katika hotuba yake alisema kwamba jeshi la Marekani la miaka 1770 liliteka viwanja vye ndege kutoka kwa Uingereza.
Hivyobasi ujumbe wake wa Twitter siku ya Jumatano kwamba wanamaji wa Marekani kuyashambulia maboti ya wanajeshi wa Iran ambayo yanahangaisha meli za kivita za Marekani ilikuwa taarifa ndogo.
Presentational white space
Lakini lilikuwa tishio kubwa la vita vya moja kwa moja kutoka kwa Marekani , tangu mauaji ya kamanda mkuu wa jeshi la Iran jenerali Qasem Soleimani mapema mwaka huu.
Mauaji hayo nusra yazushe vita vya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran. Hivyobasi tunauliza ni nini kilichomfanya rais Trump kutoa tisho hilo wakati huu?.
Na kwanini huku mataifa hayo mawili yakikumbwa na changamoto ya kukabiliana na virusi vya corona yanarudisha hali hiyo ya wasiwasi iliokuwepo?
Sababu ya moja kwa moja ya rais Trump kutoa tishio hilo inatokana na matukio ya wiki moja iliopita , wakati ambapo maboti ya wanajeshi wa Iran waliojihami yanayoendeshwa na wanajeshi wa IRGC yalihangaisha meli ya kivita ya Marekani katika Ghuba.
Meli hizo ni pamoja na USS B Puller, na The Destroyer USS paul Hamilton.
Kamanda wa IRGC jenerali Hossein SalamiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionIran iliishutumu Marekani kwa kutoa madai tofauti ya matokeo ya kisa hicho cha Ghuba
Jeshi la wanamaji wa Marekani linasema kwamba katika tukio moja , boti moja ya Iran ilipita mbele ya meli ya kijeshi ya Marekani kwa kasi.
Jeshi la IRGC lilikiri kwamba kulikuwa na makabiliano , lakini likawalaumu wanajeshi hao wa Marekani.
Kamanda wake mkuu jenerali Hossein Salami alisema siku ya Alhamisi kwamba alikuwa ameagiza wanamaji wa Iran kuliangamiza jeshi lolote la kigaidi la Marekani katika Ghuba ya Persia, kama anavyosema 'linalotishia usalama wa jeshi la Iran ama meli za raia'.
Kamanda wa IRGC jenerali Hossein Salami akizungumza na vyombo vya habari tarehe 22 April 2020Haki miliki ya pichaEPA
Image captionKamanda wa IRGC jenerali Hossein Salami aliionya Maarekani kutokabiliana na meli zake
Hofu iliopo sasa ni kwamba uadui wowote na vita vya maneno vinaweza kubadilika na kusababisha makabilianao ya moja kwa moja. Hatahivyo chapisho la rais Trump katika Twitter limebadilika kiasi.
Makamanda wa meli za kivita za Marekani katika Ghuba wana uwezo wa kuchukua hatua zozote wanazoamini zinaweza kulinda maisha yao na wafanyakazi wao pamoja na usalama wa meli zao. Wamezoea mbinu zinazotumiwa na maboti madogo ya Iran.
Lakini sehemu hii inaonyesha kwamba licha ya kuwepo kwa mlipuko wa virusi vya corona hali ya wasiwasi ya kimatifa kati ya mataifa hayo mawili bado ipo. Huenda pia ikazidishwa.
Hii ni kwasababu utaratibu wa kimkakati wa Marekani haujabadilika. Iran inataka kupunguza ushawishi wa Marekani katika eneo hilo na kupanua ushawishi wake.
Wanajeshi wakipuliza dawa ya kuuwa virusi walionekana katika gwaride la kijeshi mjini Tehran tarehe (17 April 2020)Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi wakipuliza dawa ya kuuwa virusi walionekana katika gwaride la kijeshi mjini Tehran
Shambulio la hivi karibuni la Israel nchini Syria , kwa mfano linaonesha kwamba washirika wake bado wanataka kuafikia lengo hilo .
Baadhi ya viongozi wa Iran - na kuna hatari kwamba ghasia na switofahamu zinzosababisha na Covid-19 zitaimarisha msimamo wao mkali na kuhisi kwamba huenda Marekani inayokabiliwa na mlipuko huo ikapoteza hamu ya kutaka vita katika Ghuba.
Vilevile utawala wa rais Trump unaimarisha sera yake ya kuongeza shinikizo dhidi ya Iran ukiamini kwamba kwamba mlipuko wa virusi vya corona unaweza ukasababisha kuanguka kwa utawala wa Kiislamu mjini Tehran.
Jeshi kuu nchini Iran IRGC limesema kjwamba lilifanikiwa kurusha setlaiti ya kijeshi angani siku ya Jumatano. tarehe 22 April 2020Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJeshi kuu nchini Iran IRGC limesema kjwamba lilifanikiwa kurusha setlaiti ya kijeshi angani siku ya Jumatano.
Wakati huohuo Iran inaendelea kupiga hatua katika vita vyake. Siku ya Jumatano ilizindua kile ambacho Jeshi la IRGC linasema setlaiti ya kijeshi, kwa kutumia roketi inayoonekana kutegemea teknolojia ya Korea Kaskazini , ikimaanisha kwamba mpango wake wa kinyuklia unazidi kuimarika.
Huku Iran ikiendelea kuheshimu mkataba wa nyuklia wa 2015 na mataifa yenye uwezo mkubwa duniani ambayo yalipunguza vitendo vyake vya kinyuklia , inaendelea kukiuka masharti mengi.
Ukweli ni kwamba wataalam wana wasiwasi kwamba huku hatua nyingi zilizopigwa na Iran zikiwa haziwezi kurudishwa nyuma , inajiweka katika nafasi ambayo inaweza kutengeneza centrifugues za kaboni - mashine za kuunda madini ya uranium kwa njia ya siri isioweza kubainika na wakaguzi wa kimataifa .
Rais wa Iran Hassan Rouhani akikagua teknolojia ya kinyuklia mjini Tehran tarehe (9 April 2019)Haki miliki ya pichaAFP
Image captionIran imekikuka baadhi ya vikwazo vya mkataba wake wa kinyuklia kufuatia hatua ya Marekani kujiondoa katika mktaba huo.
Mvutano kati ya Marekani na Iran usingekuwa wa kutia wasiwasi iwapo ungekuwa umepuuzwa lakini haujapuuzwa.
Na hatari ya kuzuka kwa vita vya bahati mbaya ni kubwa zaidi , hali ya kwamba mataifa yote mawili huenda hayaelewi athari za virusi vya corona na uwezo wa upinzani kuchukua hatua.

Post a Comment

0 Comments