tangazo

Mbunge wa CHADEMA alalamika kutengwa kwenye group LA WhatsApp.

Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, amelalamika kutengwa na wabunge wenzake wa Chadema kwenye kundi songezi (WhatsApp) jambo lililomfanya ashindwe kuchangia mjadala wa bajeti.


"Namshukuru Katibu wa Bunge kwa kuwasilisha ombi langu mbele yako, leo natoa mchango wangu nikiwa nimetengwa na familia ya kisiasa group la WhatsApp la chama changu, ambalo wapo viongozi wakuu wa chama changu, bila kupewa taarifa ya kukemewa au juu ya hatua hiyo iliyochukuliwa, alisema.

Amesema tangu kuanza kwa kikao cha bajeti ndiyo mara ya kwanza kusimama kuchangia baada ya kupata ridhaa ya meza ya Spika.

Post a Comment

0 Comments