tangazo

Ndege ya kijeshi ya Uturuki ikiwa na vifaa vya matibabu ya wasiri Marekani

Uturuki katika juhudi zake za kupamba na  maambukizi ya virusi vya corona  imetuma msaada wa vifaa vya matibabu na madawa nchini Marekani.

Ndege hiyo imewasili  baada ya kuanza safari yake kutoka mjini Ankara nchini Uturuki.

Marekani ndio taifa ambalo lina idadi kubwa ya watu walioathirika kwa virusi vya corona.

Ndege hiyo imewasili katika uwanja wa ndege wa  Joint Base Andrews  mjini Washington.

Ndege hiyo ilianza safari yake kuelekea nchini Marekani ikiwa na vifaa hivyo Jumanne asubuhi ikiwa na barakao, barakao maalumu kwa ajili ya wauguzi aina ya N95 na vifaa vingine ambavyo  ni muhimu katika kukabiliana ba virusi vya corona.

Post a Comment

0 Comments