tangazo

Rais Mzalendo na mpenda demokrasia, atuma salamu za Rambirambi kufuatia kifo cha Jaji Mstaafu Augustino


Leo April 28, 2020 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhan aliefariki Dunia leo Saa 2 Asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan DSMbaada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mhe Rais amesema Marehemu Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka kwa nchi yake ulioshadidishwa na umahiri wake, ukweli, Uchapakazi,  Uzalendo wa kweli.
Nakumbuka nilipokwenda kumuona hospitali mazungumzo yake yalikuwa ni ya kumtumaini na kumtegemea Mungu, kwa hiyo na mimi namuombea kwa Mwenyezi Mungu aiweke Roho yake mahali peponi Amina’- Rais Magufuli 

Post a Comment

0 Comments