Ripoti ya SIPRI- matumizi ya kijeshi yaongezeka duniani

Utafiti mpya wa Taasisi  ya  kimataifa  ya  utafiti  wa  amani (SIPRI) unasema matumizi ya kijeshi duniani kwa mwaka 2019 yamefikia katika kiwango cha juu zaidi katika kipindi cha mongo mitatu.


Utafiti mpya wa Taasisi  ya  kimataifa  ya  utafiti  wa  amani  mjini Stockholm, Sweden (SIPRI) imesema matumizi ya kijeshi duniani kwa mwaka 2019 yamefikia katika kiwango cha juu zaidi katika kipindi cha mongo mitatu. Taasisi hiyo inayataja mataifa yanayoongoza kuwa ni Marekani, China na India. 
Taasisi ya hiyo ya kimataifa yenye kuhusika na utafiti wa masuala ya Amani SIPRI imesema matumizi ya kijeshi yameongezeka na kufikia dola trilioni 1.91 kwa mwaka 2019, kikiwa kiwango kikubwa kabisa kuwahi kufikiwa kwa mwaka tangu 1988. Kiwango hicho kinaonesha ongezeko la asilimia 3.6 ikilinganishwa na mwaka 2018.
Watafiti wa SIPRI wanasema matumizi yao yanaonekana kama kuwa ni ya juu zaidi, wakigusia hali ya kuporomoka kwa uchumi kutoka na janga la virusi vya corona. Mtafiti wa tasisi hiyo Nan Tian aliliambia shirika la habari la Ujerumani DPA kwamba wanatabiri matumizi hayo yanaweza kuwa na athari kubwa kwa bajeti za mataifa katika namna yoyote ya matumizi kwa mwaka huu wa 2020 kutokana na kuzorota kwa uchumi kulikosababisha na janga la corona.

Matumizi ya kijeshi yanaweza kuathiri huduma muhimu
Aidha Tian aligusia utabiri wa Shirika la Fedha Duniani IMF kuhusu kutokea kwa kuporomoka kwa pato la ndani kwa mwaka huu wa 2020. Na kuyataka mataifa yapime matumizi kwa kutoa vipaumbele katika nyanja za afya, elimu au miundombinu ikilinganisha na matumizi ya kijeshi.
Kwa zingatio la matumizi ya mwaka 2019, mtaalamu huyo alisema Marekani inayoongoza imetumia kiasi cha dola bilioni 732, ikiwa sawa na asilimia 38 ya matumizi yote ya kijeshi duniani. China inashika nafasi ya pili ambayo imetumia dola bilioni 261, ikiwa sawa na asilimia 14 ya matumizi yote ya kijeshi ulimwenguni na India dola bilioni 71.1 na kufuatiwa na Urusi, Saudi Arabia.
Ujerumani ni miongoni mwa mataifa 10 yenye kufanya matumizi zaidi ya kijeshi.
Kimsingi mataifa matano yanayoongoza yanafanya jumla ya asilimia 62 za matumizi ya kijeshi duniani. Na katika kumi 10 kuna mataifa Ufaransa, Ujerumani, Uingereza Japan na Korea Kusini.
Matumizi kwa Ujerumani yameongezeka kwa asilimia 10, na kufikia dola bilioni 49.3. Katika mkutano wa kilele wa wa Umoja wa Kujihami wa NATO, uliofanyika Wales mwaka 2014, mataifa wanachama yalikubaliana kutumia kiasi kisichopindukia asilimia mbili ya pato lake la ndani kwa muongo ujao. Na mwaka uliopita katika pato lake la ndani Ujerumani ilitumia asilimia 1.38.
Akitoa tathmini yake mtafiti wa SIPRI Diego Lopes da Silva alisema makubaliano ya NATO yamewekwa kando barani Ulaya, na Urusi kwa mara nyingine inatazamwa kama kitisho zaidi. Kwa mwaka 2019 imetumia asilimia 4 ya pato lake la ndani katika bajeti ya kijeshi, na kulifanya taifa hilo kutumia kiasi cha dola bilioni 65.1.



Post a Comment

0 Comments