Shimo kubwa kuwahi kutokea katika tabaka la ozoni la Arctic lajifunga

Shimo la nadra kwenye tabaka la ozoni wa Arctic kabla ya kujifunga
Shimo kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika tabaka la ozoni limejifunga, ikiwa ni mwezi mmoja tu toka ligunduliwe.
Mwishoni mwa mwezi Machi, wanasayansi kutoka shirika la anga za juu la Ulaya CAMS walibaini shimo hilo kubwa katika anga ya juu ya bara la barafu lililokasjazini zaidi ya dunia la Arctic.
Baada ya muda shimo hilo likatanuka zaidi na kuwa shimo kubwa zaidi la angani kuwahi kugundulika katika anga ya kaskazini ya dunia.
Shimo hilo lilifikia ukubwa sawa wa kisiwa kikubwa cha Greenland, kilichopo baina ya Ulaya na Canada.
Lakini kufikia Aprili 23, kukawa na habari njema: "Shimo kubwa la angani la ukanda wa kaskazini wa tabaka la ozone limefikia ukomo," CAMS ilitangaza kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Kwa nini tabaka la ozoni ni muhimu?

Space photography of planet earth, showing the Arctic region and north AmericaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTabaka la ozoni linaikinga dunia na miale ya sumu kutoka kwenye jua
Tabaka la ozone ndilo linalolikinga dunia kutokana na miale hatari ya jua.
Tabaka hilo lipo baina ya umbali wa kilomita 10 mpaka 40 kutoka ardhini.
Shimo ama tundu katika tabaka hilo huathiri kuyeyuka kwa barafu duniani, kuathiri mfumo wa kinga wa viumbe hai na kuongeza hatari ya kupata saratani ya ngozi na ugonjwa wa mtoto wa jicho.
Ijapokuwa kulikuwa na matundu madogo katika tabaka la ozoni katika eneo la Arctic hapo kabla, hii ilikuwa ni "mara ya kwanza ambapo ungeweza kuzungumzia shimo kubwa katika tabaka la ozoni kwenye eneo la Arctic", kwa mujibu wa CAMS.

Tundu hilo limetokea na kutoweka vipi?

A panoramic shot of an Arctic frozen landscape, with a polar bear in viewHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMatundu ya ozoni katika ukanda wa kaskazini ya dunia ni jambo la nadra
Wanasayansi hao wanasema kuwa shimo hilo ni matokeo ya mabadiliko yasiyo ya kawaida ya hali ya hewa katika eneo la Arctic.
Pale upepo mkali unapogandisha hewa baina ya milima mikubwa ya barafu kwenye eneo hilo, hutengeneza hali ambayo wanasayansi huiita "polar vortex" ambayo ni mkandamizo mkubwa wa hewa ambao unazunguka katika eneo hilo na kuwa na nguvu kubwa ya mpaka kulichana tabaka la ozoni la eneo hilo.
Japo kwa sasa shimo hilo limejifunga, wanasayansi wanasena linaweza kujifungua kama hali ya hewa itaruhusu hilo.
"Shimo hili la ozone la eneo la Arctic halina uhusiano wowote na marufuku za kutotoka nje za virusi vya corona. Lilisababishwa na mgandamizo mkubwa na wenye nguvu wa hewa," imeeleza CAMS.
"Shimo hili ilikuwa ni moja ya dalili ya tatizo kubwa la kuharibika kwa tabaka la ozone na limejifunga kutokana na mzunguko wa kawaida wa majira yam waka, na si kupona kwa kudumu. Hata hivyo, kuna matumaini: tabaka la ozone linapona, ijapokuwa kwa kasi ndogo," limeeleza shirika hilo.

Shimo la ozone la Antarctica bado lipo wazi

A picture of Antarctica seen from spaceHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionShimo katika ukanda wa ozoni wa Antarctica huonekana kila mwaka kwa miongo mitatu sasa
Kwa upande wa kusini kabisa mwa dunia, kuna shimo kubwa zaidi ambalo limekuwa likifunguka kila mwaka kwa kipindi cha miaka 35 iliyopita.
Japo ukubwa wake hutofautiana mwaka hadi mwaka, hakuna dalili ya kujifungwa moja kwa moja kwa kipindi cha hivi karibuni.
Pia kumekuwa na kasi ndogo ya kuachana na matumizi ya kemikali za CFCs - Chlorofluorocarbons - ambazo zilipigwa marufuku mwaka 1996.
Kemikali hizo ni mbaya kwa ustawi wa tabaka hilo.
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utabiri wa Hali ya Hewa (WMO), shimo hilo la Antarctic limepungua kati ya asilimia 1 mpaka 3 kwa mwongo mmoja toka ilipotimu mwaka 2000.
Kufikia sasa, shimo dogo kuwahi kurekodiwa katia eneo hilo ilikuwa mwaka jana 2019 lakini WMO inabashiri kuwa shimo hilo halitarajiwi kujifunga moja kwa moja mpaka itakapofikia mwaka 2050.

Post a Comment

0 Comments