tangazo

Sio kila kifo kinasababishwa na Corona, acheni uzushi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ametoa rai kwa Watanzania, kuacha kutoa taarifa za uzushi za vifo kuwa kila kifo kinachotokea kinasababishwa na Virusi vya Corona.  Hayo ameyabainisha leo Aprili, 29, 2020, wakati akitoa taarifa ya mwenendo wa maambukizi ya Virusi vya Corona hapa nchini, ambapo amesema visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona vimeongezeka na kufikia 480, baada ya hii leo kutangazwa visa vipya 196, kati ya hivyo Bara ni 174 na Zanzibar ni 22.  Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa idadi ya wagonjwa waliopona nayo imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 167, Zanzibar wakiwa 36 na Bara ni 83, huku idadi ya vifo navyo ikiongezeka na kufikia 16.

Post a Comment

0 Comments