tangazo

Spika athibitisha kifo cha Ndasa ahairisha vikao vya bunge

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai leo Bungeni amethibitisha kwamba ni kweli Mbunge wa Sumve Richard Ndasa amefariki dunia.

“Bunge letu limepata msiba mwingine mkubwa wa kuondokewa na Mbunge mwenzetu, mbunge wa jimbo la Sumve, Richard Ndasa ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo 29 April 2020 hapa Dodoma”

“Kufuatia msiba huo taratibu za mazishi zimeanza kufanyika, kwa siku ya leo hatutaendelea na kikao cha Bunge badala yake tutakuwa na maombolezo ya msiba wa mwenzetu aliyekua Mbunge wa Jimbo la Sumve kwa vipindi vitano” - Job Ndugai

Ni siku 8 zimepita toka Mbunge mwingine afariki dunia ambaye ni Mama Mch. Gertrude Rwakatare aliyefia Dar es salaam na kuzikwa na kwenye eneo la kanisa lake.

Post a Comment

0 Comments