TAKUKURU yarejesha Mil.74 walizopigwa walimu wastaafu


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mara (TAKUKURU) imefanikiwa kurejesha jumla ya kiasi cha shilingi Milioni 74 kwa waalimu wanne kutoka taasisi za mikopo umiza.

Akizungumza wakati akirejesha fedha hizo Kamanda wa TAKUKURU Mkoa Alex Kuhanda amethibitisha kuwepo baadhi ya watumishi wa serikali ambao ni makatibu wa tume ya Utumishi wa walimu kuthibitika uhusika wao katika uwakala wa ukopeshaji.

Kamanda Kuhanda, ameeleza kuwa moja kati tuhuma ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu alibeba hundi ya mafao ya mstaafu kutoka Mara mpaka Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambako alilazwa mstaafu Sareta Masawa ambaye kwa sasa ni marehemu na kushughulikiwa kibari cha kumtoa kisha kumpeleka benki moja wapo jijini Mwanza kisha kumpora kiasi cha shilingi milioni 13.

Pia amesema kuwa kuna wastaafu wawili ambapo mmoja anatambulika kwa jina la Prisca Odoyo, alikopa Tsh 1,400,000/= ili ilipe Tsh 3,000,000/= pensheni yake kiasi cha Tsh 99,000,000/= ilipotoka akajikuta anaporwa jumla ya Tsh 86,000,000/= sawa na asilimia 86.9 ya pensheni yake huku riba ikiwa asilimia 6143, ikiwa na maana kuwa pensheni yake ya Tsh 99,000,000/=, aliyoifanyia kazi kwa zaidi ya miaka 30 aliambulia Tsh 13,000,000/= tu. ambapo TAKUKURU imefanikiwa kurejesha kiasi cha Tsh 37,000,000/=

Pia mkopeshaji wa pili alimkopesha Tsh 6,000,000 pensheni ilipotoka mstaafu akajikuta anaporwa Tsh 25,000,000/= sawa na asilimia 417 ambapo wakopeshaji wamewahi kuwa na uhusiano wa kiukopeshaji na mwalimu mstaafu ambaye ni mlemavu wa viungo, ambapo si kwa viwango hivyo. Ambapo ofisi inaendelea na uchunguzi ila atarejeshewa kiasi cha Tsh 11,000,000/= kama sehemu ya marejesho yaliyofanywa na wakopeshaji umiza baada ya TAKUKURU kuingilia kati.

Aidha amefafanua kuwa mstaafu mwingine alikopa Tsh 2,000,000/= ili arudishe Tsh 4,000,000/= ili pensheni yake ilipotoka akajikuta kulipa Tsh 13,000,000/= sawa na asilimia 670.

Hata hivyo Kamanda huyo katoa angalizo kwa watumishi wa umma walio na dhamana ya kusimamia fedha na vitu vinavyoletwa kwa ajili ya kupambana na gonjwa la COVID-19 kutozitumia raslimali hizo kwa maslahi yao binafsi.

Post a Comment

0 Comments